MTANZANIA ATOLEWA BIG BROTHER

   Matumaini ya watu wengi kumuona mshiriki  kutoka Afrika Mashariki ndani ya jumba la Big Brother Africa kuibuka na ushindi, yameshuka kwa kiasi kikubwa baada ya washiriki kutoka nchi mbili za Afrika Mashariki kutolewa nje ya jumba hilo.

Wiki moja baada ya washiriki Lillian kutoka Nigeria, Esther kutoka Uganda na Sabina kutoka Kenya kutolewa kwenye mjengo huo, Mtanzania Laveda aliyekuwa na mahusiano ya karibu na Permithias pamoja na Mkenya Alusa wamekutana na ‘rungu’ la kura lililowatupa nje ya jumba hilo.


Laveda anakuwa mshiriki wa sita wa jinsia ya kike kutolewa nje ya jumba la BBA huku Alusa akiwa ni mshiriki wa kwanza wa kiume kutolewa Big Brother Hotshots.




Aliekuwa mshiriki wa Tanzania Laveda kwenye Big Brother Hotshots 2014.


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA