ROSE MUHANDO NI MGONJWA, AOMBA RADHI NA KUAHIDI KURUDISHA PESA



Staa mkubwa wa Injili Bongo, Rose Muhando.
      TUMUOMBEE! Hali ya kiafya ya staa mkubwa wa Injili Bongo, Rose Muhando siyo nzuri na amewaomba Watanzania wamuombee kwani ni mgonjwa.
     Rose ambaye ameripotiwa kwa misala tofauti ya kuchikichia fedha za shoo hivi karibuni, amefunguka kuwa afya yake si nzuri kwani anasumbuliwa na mshipa kwenye mguu, akafanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Mkoa ya Dodoma.
“Siko vizuri kiafya nimefanyiwa upasuaji mguuni, nimeshonywa nyuzi nne lakini bado hali yangu si nzuri kiafya, nawaomba Watanzania waniombee,” alisema Rose kwa tabu na kuongeza:
“Hata ukiniona utanihurumia kwani mbali na upasuaji kwenye kidole gumba pia nimevimba sana uso.
“Kwa sasa nipo kitandani nyumbani kwangu najiuguza. Nitarudi tena hospitalini Jumanne ijayo.”
Kuhusu suala la kudaiwa kuingia mitini na fedha tofauti za shoo, Rose ameomba radhi kwa Watanzania.
“Nawaomba sana radhi wote niliowakosea, niwaombe waniombee nipone na nitarejesha fedha zao,” alisema Rose.
Tunamuombea Rose kwa Mwenyezi Mungu ampe afya njema ili aendelee na huduma ya kumtumikia Mungu kwa njia ya nyimbo za Injili.

Chanzo Gazeti la Risasi

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA