SIMBA YAMKATIA TAMAA KIONGERA


                                          Paul Kiongera

             Kufuatia kuwa na majeraha yatakayochukua muda mrefu kurudi uwanjani, timu ya Simba imemkatia tamaa mshambuliaji wake Paul Kiongera ambaye anatarajiwa kuwa njkwa wiki sita. Kiongera aliumia goti katika mechi ya ligi kuu Bara dhidi ya Coastal Union ambapo imeelezwa kuwa maumivu ya goti lake ni ya muda mrefu lakini alikuwa na nafuu kabla ya kutua Simba, hivyo safari hii anaweza kuwa nje kwa muda mrefu na kukosa mechi nyingi za Simba.
         Daktari wa Simba Yassin Gembe, alikuwa ni mmoja wa madaktari waliyomfanyia uchunguzi na kubaini majeraha makubwa ya mchezaji huyo. Lakini taarifa zinaeleza kuwa benchi la ufundi la timu hiyo limeshakata tamaa kuwa naye hivi karibuni.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA