PHIRI ASHTUKIA JEURI YA MAXIMO


KOCHA wa Simba, Patrick Phiri.
KOCHA wa Simba, Patrick Phiri, amesema Yanga wala isijigambe kwamba ina timu nzuri katika Ligi Kuu Bara kwani jeuri ya kikosi chao kinachofundishwa na Marcio Maximo ni mabeki Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ basi.
Kisa cha Phiri kutoa kauli hiyo ni mitazamo wa wadau wa soka ambao wanadhani Yanga ni bora kuliko Simba iliyotoka sare mara nne na kushika nafasi ya tisa katika Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi nne katika mechi nne.
Phiri ambaye Jumamosi timu yake haikufungana na Yanga alisema: “Unadhani Yanga inapata jeuri kutokana na kitu gani? Ni ile beki yake inayoundwa na Yondani na Cannavaro na si vinginevyo, mabeki wale wamecheza pamoja kwa muda mrefu hivyo wanaweza kukabiliana na mshambuliaji yeyote yule.”
Kocha huyo alisema hata katika mechi yao iliyopita mabeki hao ndiyo waliozuia ushindi wa timu yake kwani walimudu kuwazuia washambuliaji wake Emmanuel Okwi na Elius Maguli aliyekuwa “Tazama katika mechi nyingi mabeki hao ndiyo wanaofanya kazi kubwa ya kulinda lango la Yanga, lakini akikosekana mmoja tu utaona timu itakuwa haifanyi vizuri, hawa ndiyo wenye majaliwa ya Yanga na wanacheza vizuri kwa kweli,” alisema Phiri.
Alisema mabeki hao huweka mazingira mazuri ya kipa wao Deo Munishi ‘Dida’ kuonekana bora kwani mara nyingi hawaruhusu washambuliaji hatari kuingia na mipira ndani ya eneo lao la hatari.
Phiri akaongeza kwa kusema ubaya wa mabeki hao wapo vizuri kwa kucheza mipira yote ya juu na chini na hata ile ya kutumia ubabe kuanzia mwanzo hadi mwisho kitendo kinachowaogopesha washambuliaji wa timu wanazokutana nazo.
“Wanamudu kila aina ya mchezo kama mkiwachezea mipira ya chini wapo, juu wapo na hata ukitumia nguvu na kasi pia wanacheza sasa hawa ndiyo wanaoifanya Yanga kuwa imara muda wote,” alisema Phiri ambaye ni raia wa Zambia.
Katika mchezo dhidi ya Simba, Cannavaro alicheza akiwa ameshonwa nyuzi tatu usoni baada ya kuumia katika mechi ya Taifa Stars na Benin na nyuzi hizo zilitolewa Jumatatu ya wiki hii na alimudu kuwazuia Okwi na Maguli.
Hata hivyo mabeki hao wameruhusu mabao manne huku safu yao ya ushambuliaji nayo ikifunga mabao manne tu katika mechi nne za ligi kuu. Keshokutwa Jumamosi Yanga inatarajiwa kucheza na Stand United mjini Shinyanga katika mwendelezo wa ligi hiyo.
Yanga imeweka kituo cha muda Dodoma na leo Alhamisi jioni itajipima na CDA. kwa mabavu na mabeki hao.


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA