MESSI AGOMA KUTOLEWA BARCELONA

                           Lionel Messi 
SUPASTAA wa soka, Lionel Messi, ameripotiwa kumgomea kocha wake Luis Enrique wakati alipotaka kumtoa kwenye mechi kati ya Barcelona na Eibar.
Gazeti la AS linaripoti kwamba kocha huyo wa Barca wakati kikosi chake kikiwa mbele kwa mabao 3-0, alipanga kumtoa Messi ili amwingize Munir El Haddadi kwenye dakika ya 76.
Luis Enrique alisimama nje ya mstari na kuonyesha ishara kwamba Muargentina huyo anapaswa kutoka, lakini Messi aligomea amri ya kocha wake na kuendelea kubaki uwanjani.
Baada ya kuona mpango huo umekwama, Enrique aliamua kumtoa Neymar na kumwingiza Munir.
Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Enrique alisema: “Ni lazima niweke sawa kila kitu, lakini naamini katika hisia zangu.
“Kwa msimu wote uliobaki, mambo mengine ni muhimu. Lakini, nadhani kwa sasa kitu muhimu ni timu na pia Messi mwenyewe.
“Wakati mwingine ninaposimama kwenye mstari na kutazama uwanjani, huwa nawaza sana na kukiri tuna bahati kwa kuwa na Messi kwenye timu yetu.”
Juzi Jumanne kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Barcelona iliichapa Ajax mabao 3-1.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA