WAISLAMU WAHISI KUONEWA NA SERIKALI, NI KUTOKANA NA ASKOFU GWAJIMA KUACHIWA KWA DHAMANA WAKATI SHEHE PONDA AMENYIMWA DHAMANA HADI LEO

SIKU chache kupita baada ya Mkutano wa 19 wa Bunge kumalizika,na serikali kuutupia mbali mswaada wa sheria ambao unaruhusu kuwepo makakama ya Kadhi nchini kutajadiliwa kwenye mkutano huo, Nayo Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini wameibuka na kutoa tamko zito kwa kuwataka waislam wote nchini kutoshiriki kwenye kura ya maoni ya kupitisha katiba pendekezwa Bunge Maalum la Katiba,kwa madai kwamba serikali haina nia nzuri na waislam nchini kwa kitendo chake cha kukataa kuwepo mahakama ya Kadhi nchini. Vilevile Taasisi hiyo imewataka pia waislam wote kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura na kujiandaa kufanya uamuzi mgumu ambao wanasema hajawai fanywa na waislam nchini tangu taifa kupata Uhuru. Akisoma Tamko hilo lenye kura sita jana jioni kwenye msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Jijini Dar es Salaam ,Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislam nchini Sheikh Mussa Kundesha kwa niaba ya asasi za kiislam 11 zinazounda umoja huo na kushuhudiwa na Mamia ya waumini wa dini hiyo pamoja waandishi wa Habari ambapo Sheikh Kundesha alisema- Waislam wote nchini wamechoka na uonevu wanaodai kufanyiwa na Serikali iliyoko madarakani kwa kitendo cha kuondo Mswaada wa Mahakama ya kadhi Bungeni ambapo alisema ni kuendelea kuchochea vita ya kidini nchini. “Kuna kila sababu ya kuamini kuwa Serikali ya CCM imeshindwa kulishughulikia suala la mahakama ya Kadhi katika uhalisia wake kama ilivyoahidi kupitia ilani yake kwenye uchaguzi ibara ya 108 (b) mwaka 2005 na sasa inafanya hadaa za kisiasa kuwadanganya waislam ili waonekane inalishughulikia suala la mahakama ya Kadhi kama walivyoahidi” “Kwa ubabe huu wanaotufanyia waislam sasa tunawaomba waumini wote wa kiislam nchini kutoipigia kura katiba pendekezwa kwasababu sio katiba nzuri kwa waislam harafu tunawataka kila mmoja aliyetimiza miaka 18 ajiandikishe kwenye Daftari wa wapiga kura kujiandaa kufanya uamuzi mgumu ambapo utalitikisa nchi”alisema Sheikh Kundesha. Alisema kuwa kitendo cha Serikali kuwatambua Makadhi wa Bakwata pamoja wanachosema ni ‘Mahakama hewa ya Kadhi’ chini ya Bakwata ni kinyume na Katiba ya nchini ibara 19(1) na (20) kwa kuwalazimisha waislam wawe chini ya Bakwata ambapo wanasema hawatakubaliana nalo. KUHUSU TAMKO LA MAASKOFU. Pia katika Tamko la Taasisi hiyo kiislam ambapo litasomwa kila msikiti Ijumaa wiki hii nchi nzima pia wamezungumzia Matamko mawili yaliyotolewa Jukwaa la kikiristo nchini ambapo Taasisi hiyo ya Kiislam wameonyesha masikitiko yao kwa kusema ni dhahili hapa nchini kuna serikali dhaifu kwa kuwaacha maaskofu kutoa matamko ambayo wanadai ni ya kichochezi. “Ushahidi kwamba ni chuki tu husda ni pale ambapo hata waislam tuliopendekeza mahakama ya Kadi iwekwe kwenye Katiba pendekezwa,lakini tunashangaa hawa maaskofu wamekuwa wakiipinga Mahakama hii wakati hii dini tofauti na y a kwao na sisi waislam tumewavumilia lakini tunahoji hawa maaskofu wanataka nini” KUHUSU KESI ZA MASHEIKH NA KUNYIMWA DHAMANA. Pia Taasisi ya Kiislam wameonyesha kuchukizwa kwa kitendo cha Masheikh mbalimbali akiwemo shehe Ponda ambao wapo mahabusu na kunyimwa Dhamana na Serikali ila wanashangaa kitendo cha Serikali kuwamwachia Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Askofu Josephat Gwajima wanadai kitendo hicho kinaonesha Serikali kuwapendelea wakristo. “Masheikh mbalimbali wako mahabusu wakinyimwa Dhamana bila sababu za msingi kwa kesi za uchochezi au kwa kisingizio cha Ugaidi wakati huo huo tumeshuhudia Maaskofu wakitoa kauli za uchochezi pasina kuchukuliwa hatua yeyote ikiwemo sakata la Askofu Gwajima” KAMPENI WANAO DAI KUUA MADRASA. Pia Taasisi hiyo wamezungumia kitendo cha Serikali kuwakamata wa Mashehe mbalimbali wanaowafundisha watoto majumbani kwa madai ya serikali kutofuata taratibu za mafunzo likiwemo matukioa tofauti yaliyotokea mkoani arusha- Kwa kusema ni wazi serikali imejitosa kuua madrasa nchini. “Lakini Takriban mwezi mmoja sasa,njama hizi za kuua madrasa zetu zimeibuka kwa kasi kubwa na nguvu kwa kuendesha kamatakamata ya waalimu wa madrasa zao katika hali duni majumbani mwao wakifundisha Quran na mafunzo mengine ya Uislam kama tulivyoshudia huko mkoan Moshi na Arusha” “Tunataka Serikali itusaidie kufundisha Elimu ya dini ya Kiislam kwa mujibu wa sheria ndiyo ipi,sheria hiyo ilipitishwa lini na Bunge lipi?kwa mujibu wa Katiba ya nchi ibara 20 (1) kazi ya kutangaza dini ni suala binafsi,iweje sasa Serikali inakuja na madai haya ya kufundisha dini kinyume na Sheria kwa walimu wetu wa madrasa”

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA