KUTANA NA MWANAHARAKATI PETER LUSSE AMBAE HAOGOPI WALA HACHOKI KUKPIGANIA KILE ANACHOKIAMINI KUWA NI BORA

Siku zote shetani akiwa anataka kukukatisha tamaa huwa anatuma viwakala vyake vidogo vidogo ili kukujaribu, lakini unapokuwa strong na kumuonyesha kuwa haumuogopi ndipo anakuja yeye mwenyewe mzima mzima ili kukutishia, lakini ukimpuuzia na kumuona kama anayoyaleta ni mambo ya kitoto ataondoka na kukuaha ila hatocheza mbali na wewe kwasababu lengo lake ni kukuvunja moyo, ila ukionyesha kumuogopa moja kwa moja utakuwa umekubaliana na mkakat wake na ana uwezo wa kukupoteza within a minute.... Hiyo ndiyo kanuni ya maisha.

Peter Lusse ni mmoja miongoni mwa watumishi wa Mungu wanaopambana sana kufikia ndoto zake ingawa sometimes upinzani mwingi unajitokeza lakini hakati tamaa kwasababu anamjua Mungu aliyemtuma. Ni miongoni mwa wahasisi wa Gospel Movie ukiachilia mbali Jenifer Mgendi ambao wanakuja kwa kasi sana katika kuliteka soko la movie Tanzania kwa jinsi anavyofanya kazi zenye ubora. Hadi sasa ameshatoa movie mbili ambazo zinafanya vizuri sana sokoni, ambazo ni Agano aliyoitoa mwaka 2014, pamoja na Behinde The Pastor's aliyoitoa mwaka 2015. Movie hizo ziko sokoni zinasambazwa na wadosi wa Umoja Vision ambapo zinaonyesha kutikisa sokoni.

Mbali na fani ya kuigiza Peter Lusse ni muimbaji mkongwe ambae anamtumikia Mungu vilivyo katika kipaji chake cha uimbaji, alizindua album yake ya kuteleza sio kuanguka mwaka 2009 katika ukumbi wa Msimbazi Centre na kwa kuwa ni Mtumishi anaependa kufanya vitu kwa ubora alihakikisha hata matangazo na ukumbi alioutumia vinamtukuza Mungu kwa njia ya Qality.

Mbali na album hiyo ya kuteleza sio kuanguka Peter Lusse ana album zingine 3 ambazo ni matata sana, kama vile Kiungo aliyoitoa mwaka 2006, Kibao aliyoitoa mwaka 2010, pamoja na album ya Mwache aende zake aliyoitoa mwaka 2013, ambapo ndani ya album hii ana track yake moja kali sana inayoitwa leo ni siku njema.

Blog ya nyumbani tunampongeza sana Peter Lusse kwa kufanya kazi zenye ubora, na wewe hakikisha unapata nakala ya nyimbo zake pamoja na Filamu zake ambazo ukizitazama lazima zitazaa kitu cha kimungu ndani yako. 

We wish you all the Best kamanda....

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA