HALI ILIVYOKUWA NYUMBANI KWA GWAJIMA LEO



Askari wakiwa nyumbani kwa Gwajima.
  
Makamanda wa polisi wakiwa tayari kwa lolote.
  
Gari lililombeba Gwajima likitoka ndani ya nyumba yake kuelekea kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano.

Mawakili wa Gwajima wakisalimiana na mmoja wa maofisa wa polisi mara baada ya kufika eneo la tukio.
  
Waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio.

Waumini wa Gwajima wakiwa wamezunguka nyumba wa askofu wao.
  
Kundi la wafuasi wa Gwajima wakifika nyumbani kwake mara baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.
  
Baadhi ya watu waliokuwemo ndani ya nyumba ya Gwajima wakichungulia dirishani.
 
****
Wakati  taarifa zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya jamii kuwa nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, imezingirwa na polisi, habari kamili ni kwamba zoezi la kumkamata askofu huyo lilishindikana baada ya kugoma kufungua geti lake.
 
Polisi hao waliokuwa na silaha walifika nyumbani kwa askofu huyo maeneo ya Salasala jijini Dar wakiwa kwenye magari zaidi ya manne ambapo walipiga kambi katika eneo hilo kwa saa sita huku njia hiyo ikiwa imefungwa kwa saa kadhaa kabla ya waandishi wa habari na baadhi ya waumini wa askofu huyo kuruhusiwa kupita.
 
Hata hivyo baada ya polisi hao kuzungumza na mawakili wa Gwajima na viongozi kadhaa wa kanisa hilo, waliamua kuondoka huku wakitoa amri kiongozi huyo afike kituo kikuu cha polisi  kwa ajili ya mahojiano zaidi ambapo alifika na baadaye kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu ambapo alisomewa  mashitaka  mawili  ya  kutoa lugha ya matusi na kushindwa kutunza silaha.
  
Askofu  huyo  ameachiwa  kwa  dhamana  na  kesi  yake  itaendelea  Mei 4  mwaka  huu.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA