MGOMO WA MABASI: MWANZA KWENDA MUSOMA LAKI NNE



Abiria zaidi 1000 waliokuwa wakisafari kutoka Musoma kwenda Dar es salaam kupitia mikoa ya Mwanza na Shinyanga na wale wa kwenda mpakani mwa Tanzania na Kenya Sirari pamoja na wa ndani ya mkoa wa Mara wameshindwa kusafari baada ya madareva kuitisha mgomo.

Baadhi ya madereva ambao wamekutwa katika kituo kikuu cha mabasi ya Bweri mjini Musoma,wamesema kuwa mgomo huo umeitishwa kwa ajili ya kupinga agizo la serikali la kukataa kusajili upya leseni zao hadi baada ya kwenda kusoma katika vyuo vinavyotambulika serikalini.

Kwa upande wao baadhi ya abiria wamesikitishwa na mgomo huo wa madereva ambao umesababisha hata wagonjwa kushindwa kusafiri hivyo wameitaka serikali kuchukua hatua za kumaliza migomo hiyo ambayo wamesema imekuwa kero kubwa kwa wananchi.

Abiria hao wameshuhudiwa wakiwa wamesimama kwa makundi katika kituo hicho kikuu cha mabasi huku magari makubwa ya abiria yakishindwa kuingia kabisa kituoni hapo hatua ambayo imesabisha baadhi ya abiria kulazimika kukodisha magari madogo aina ya taxi kwenda jijini Mwanza kwa gharama ya shilingi laki nne kutoka laki mbili za kawaida.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA