ALSHABAAB WASHAMBULIA JENGO LA WIZARA YA ELIMU MOGADISHU

Maofisa wa Polisi nchini Somalia wakiingia ndani ya jengo lililovamiwa na Al Shabaab ili kukabiliana nao.
Watu 17 wameripotiwa kuuawa katika jengo ya Wizara ya Elimu mjini Mogadishu, Somalia. Vyombo vya habari mjini Mogadishu vimeripoti kuwa wavamizi hao walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo la waizara ya elimu nchini humo.
Kabla ya wavamizi kadhaa kuingia ndani ya jengo walianza kwa  kupiga risasi za kutishia, kisha kulipua bomu na risasi ziliendelea kusikisa ndani ya jengo hilo wakati Al Shabaab wakitekeleza unyama huo wa kutisha.
Msemaji wa wa kitengo cha mashambulizi cha kundi la wapiganaji wa Al…
Maofisa wa Polisi nchini Somalia wakiingia ndani ya jengo lililovamiwa na Al Shabaab ili kukabiliana nao.
Watu 17 wameripotiwa kuuawa katika jengo ya Wizara ya Elimu mjini Mogadishu, Somalia. Vyombo vya habari mjini Mogadishu vimeripoti kuwa wavamizi hao walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo la waizara ya elimu nchini humo.
Kabla ya wavamizi kadhaa kuingia ndani ya jengo walianza kwa  kupiga risasi za kutishia, kisha kulipua bomu na risasi ziliendelea kusikisa ndani ya jengo hilo wakati Al Shabaab wakitekeleza unyama huo wa kutisha.
Msemaji wa wa kitengo cha mashambulizi cha kundi la wapiganaji wa Al Shabaab Sheikh Abdiasis Abu Musab, amethibitisha kuwa ni wao waliotekeleza shambulizi hilo na kuwa ''wapiganaji wetu wamekwisha ingia ndani ya jengo hilo la wizara ya elimu''.
Kutokana na ripoti ya Polisi mjini Mogadishu inasema, mapigano yanaendelea hadi sasa ndani ya jengo hilo baina ya majeshi ya serikali na wapiganaji.
Wapiganaji wa Al Shabaab wametekeleza mashambulizi kama haya katika siku za hivi punde katika Chuo Kikuu cha Garissa mjini Nairobi nchini Kenya na kuuwa watu wapatao 150 huku wakiacha mamia ya majeruhi wakiendelea kuugulia wakati huo wapiganaji wote watano wa al shaabab wakiuawa na jeshi la serikali nchini Kenya.
Mwezi uliopita wapiganaji wa Al Shabaab walishambulia hoteli moja mjini Mogadishu uvamizi huo ulikamilika siku mbili zilizofwatia.
Waandishi wa habari walioshuhudia matukio kabla ya uvamizi huo wanadai kuwa kulikuwa na milipuko miwili mikubwa kabla ya milio ya risasi kuanza kusikika kutoka jengo hilo. Hakuna kundi lililothibitisha kutekeleza shambulizi hilo lakini Al Shabaab imekuwa ikitumia mbinu kama zilizotumika leo.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, kundi hilo la waislamu la Al Shabaab linapinga serikali iliyoko sasa ambayo inaungwa mkono na majeshi ya Umoja wa Afrika.
 CHANZO NA BBC

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA