MAJAMBAZI YAVAMIA GARI LA BONITE MOSHI, YAUWA DEREVA NA MLINZI NA KUPORA MAMILIONI


Mlinzi wa Kampuni ya Bonite, aliyetambulika kwa jina la Edson Shamba baada ya kupigwa risasi na majambazi mjini Moshi.
  
Dereva wa Kampuni ya Bonite aliyetambulika kwa jina  la Amini Mselemu mara baada ya kushambuliwa kwa risasi na majambazi.
  
Tarehe 20/04/2015, majira ya saa 12 jioni, katika eneo la Soweto ya chini eneo la Radio Kli Fm, Kata ya Soweto, Tarafa ya Moshi Magharibi, Wilaya ya Moshi, gari la Bonite lenye usajili wa namba T.803 ATR aina ya Toyota Hiace lililotoka kwenye makusanyo ya fedha za mauzo lilivamiwa na majambazi wapatao wanne wakiwa na Bastola huku wakitumia usafiri wa pikipiki mbili aina ya Boxer na Srm.

Katika tukio hilo mtu aitwaye Edson Shamba(56), Mnyiramba mkazi wa matindigani ambaye alikua ni mlinzi na alikua akisindikiza gari hilo akiwa na bunduki aina ya Short Gun namba 8710653 ikiwa na risasi tano aliuwawa papo hapo kwa kupigwa risasi maeneo ya kichwa, ambapo Amini Mselemu(61), Mnyao, mkazi wa mtaa wa Chunya Moshi aliyekua dereva wa gari hiyo, alipigwa risasi maeneo ya kifuani, tumboni, mkononi na alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu usiku wa jana katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo mjini Moshi.

Majambazi  hao  walipora  fedha  yote  ya  mauzo  ambayo  thamani  yake  bado  haijajulikana    na  kisha  kutokomea  kusikojulikana.

Watu  wanne  ambao  ni  wakala  wa  mauzo  wa  kampuni  hiyo  wanashikiliwa  na  polisi  kwa  ajili  ya  mahojiano. Watu  hao  walikuwa  ndani  ya  gari  hilo  wakati  wa  tukio.

Miili yote ya marehemu imehifadhiwa katika hospital ya rufaa ya KCMC mjini Moshi na jeshi la polisi linaendelea na kuwatafuta wahusika ili kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Imetolewa  na :
G.Y. Kamwela-SACP,
Kamanda  wa  Polisi  Wa  Mkoa  wa  Kilimanjaro.


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA