GODBLESS LEMA AMSHAMBULIA ZITTO KABWE, AMTUHUMU KUIKOSESHA USHINDI CHADEMA
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewatoa hofu wanachama wake mkoani Shinyanga kikidai propaganda zinazoenezwa na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Bw. Zitto Kabwe, anayedai chama hicho kimepoteza mwelekeo si za kweli bali ni uongo. Mbunge wa Arusha Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa, Bw. Godbless Lema, aliyasema hayo hivi karibuni mkoani Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mahakama ya Mwanzo. Alisema chama chao bado kipo imara na hakitagawanyika kama inavyodaiwa na Bw. Kabwe ambaye CHADEMA kilimfukuza katika chama baada ya kukisaliti hivyo kukiuka Katiba ya chama hicho. "Ndugu zangu wana Shinyanga, CHADEMA tupo imara na tutaendelea kuwa imara hadi tukamate dola na kuwakomboa Watanzania ambao wanateseka tangu tupate uhuru. "Zitto hana ubavu wa kukigawa chama chetu kama anavyofikiri na kuamini...anahangaika bure, alitaka kukiua tukamshtukia na mimi ndiye mtu wa kwanza kubaini njam...