WANAFUNZI WATATU NCHINI INDIA WAMEGONGWA NA TRENI NA KUFARIKI WAKIJARIBU KUPIGA SELFIE





Upigaji wa picha kwa njia ya Selfie umeendelea kuwa gumzo dunia nzima na kufanya ongezeko la ununuaji wa simu za smartphone kuongezeka kwa wingi.

Wanachuo watatu huko New Delhi, India Yakub, Afzal, na Iqbal wamepoteza maisha baada ya kunogewa kupiga picha za selfie katika barabara ya treni na kufariki hapo hapo.


Kwa mujibu wa polisi walisema mmoja wa wanafunzi hao ambaye alinusurika kufa alisimulia kuwa walikua wakisafiri kwa gari kwenda kwenye mji wa Agra, na baadaye kuamua kushuka eneo la treni kwa lengo la kupiga selfie huku yeye akiwapiga picha ili kuziweka kwenye mitandao ya kijamii ambapo wakiwa hawajui kinachoendelea treni ilikuja kwa kasi na wote watatu kufariki.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI