VURUGU ILULA MKOANI IRINGA POLISI WAUWA, WANANCHI WACHOMA MOTO KITUO CHA POLISI






Inasemekana polisi walivamia eneo la kilabuni na kuanza kupiga kila raia na kusababisa kifo cha huyo mama muuza Pombe za kienyeji. Kosa ni kufungua kilabu cha Pombe kabla ya muda ulioruhusiwa kisheria.

Wananchi wamechoma matairi barabara Kuu hakuna gari inayopita, Polisi bado hawajafika waliopo wamekimbia baada ya kuzidiwa na wananchi.


Baadae gari tatu zilizosheheni FFU zimewasili mabomu yanapigwa mfululizo, sasa hivi wanasafisha barabara kwa kuzima moto na kutoa matairi njiani.
WANANCHI wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa, wamevamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea leo asubuhi kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina lake kujigonga ukutani na kuanguka kisha kufariki dunia wakati akiwakimbia polisi waliokuwa kwenye oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.

Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita, hali iliyosababisha polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la Nyagawa.

Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI