MAMIA WAMZIKA BABA YAKE DULLY SYKES



Baba wa staa wa muziki Dully Sykes, Marehemu Abby Sykes aliyefariki dunia juzi katika hospitali ya taifa Muhimbili amezikwa jana katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.

Msiba huo mkubwa katika tasnia ya Burudani umeweza kugusa mamia ya waombolezaji wakiwepo mastaa mbalimbali na wadau wa sanaa hiyo, ambao walimfahamu marehemu kutokana na shughuli zake za muziki.
  
 Dully Sykes alisema hili linakuwa ni pengo kubwa sana kwake, akimchukulia baba yake kama mwalimu, kiongozi na rafiki ambaye ndiye amemfanya yeye kuendesha maisha yake kupitia muziki.
  

Wasani mbalimbali pia waliweza kujitokeza katika msiba huo akiwepo Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salam, Mhe Said Mecky Sadick, Jaji Warioba, Jaji Othman Chande, Miraji Kikwete na wengine wengi ambao hawakuacha kutaja wasifu wa marehemu wa kuwa mtu wa watu hususan rafiki wa vijana.
  
Mpekuzi tunaitakia faraja familia ya Abby Sykes na wote wale walioguswa na msiba huo, Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI