SUTI YA WAZIRI WA KILIMO, KILIMO NA USHIRIKA YAGEUKA GUMZO BAADA YA KUKOSEWA KUFUNGWA VIFUNGO


Suti  ya  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh Steven Wassira  imegeuka  gumzo  mtandaoni baada  ya  kukosewa  kufungwa  vifungo  vyake.....

Wassira  alionekana  ndani  ya  vazi  hilo wakati  wa   Sherehe za Utume zilizoandaliwa na kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) na kujumuisha nchi zingine 11 za Afrika Mashariki na Kati.
 
Sherehe  hizo  zilizofanyika  juzi uwanja wa taifa  Dar  zilihudhuriwa  na kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson ambapo mgeni rasmi  wa  sherehe  hizo  alikuwa  ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh Steven Wassira (wa pili toka kushoto) akiwa katika  picha ya pamoja  na  kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson( wa  nne toka kushoto) wakati wa sherehe za utume wa kanisa  hilo.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI