KUJIFUNGUA KWA FLORA MBASHA MKE/MUME KIGUGUMIZI, WASIKILIZE HAPA

Picha mbalimbali zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiuonyesha mwimbaji wa nyimbo za injili Florah Mbasha akiwa leba akijifungua zimezua utata baada ya aliyekuwa mumewe Emmanuel Mbasha kupata kugugumizi kwa kutotoa majibu ya uhakika aliulizwa kuhusiana na kujifungua kwa mkewe huyo. Mbasha amehojiwa na Soudy Brown kupitia Uheard hakutoa majibu ya kuelewa baada ya kila anachoulizwa anajibu kwamba hamsikii kwamba ndiyo alikuwa anaaamka na simu ikakata. Kumekuwa na sintofahamu kuhusu mimba ya Florah na mtoto aliyejifungua kwani wakati mwimbaji huyo alipokuwa mjamzito walikuwa na mgogoro mkubwa wa kifamilia hadi kufikia ya kuomba talaka mahakamani. Mbasha alikuwa akilalamika kuwa mkewe huyo alikuwa na mahusiano na askofu na kwamba alimpa gari na kumpangia nyumba maeneo ya Mbezi hivyo kutoelewaka mimba hiyo niya Mbasha au ya Askofu. Hata hivyo Florah Mbasha alipoulizwa kuhusu picha hizo na kujifungua alisema kuwa alishajifungua muda mrefu na anashangaa picha hizo kuonekana hivi karibuni,alipoulizwa kama ujauzito ni wa mumewe au Askofu hakujibu akakata simu.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI