LIPUMBA ASITISHA MAANDAMANO YA VIJANA CUF



Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF)  Profesa Ibrahim Lipumba leo amewasihi Jumuiya ya Vijana wa CUF(JUVICUF) kusitisha maandamano kama jeshi la polisi lilivyoagiza .
 
Akizungumza leo katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni, jijini Dar e s Salaam,  amesema kuwa vijana hao waache kuandamana kwa sababu kunaweza kutokea madhara makubwa ikiwa ni pamoja na  kupigwa risasi, vifo na kadhalika.
 
Alisisitiza waache kuandamana ingawa dhamira yao  ya kuitaka  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iongeze siku za uandikishwaji wa upigaji kura  kutoka siku saba hadi 14 ina mantiki kwa Watanzania wote. 
 
JIVICUF walikuwa waandamane kusisitiza, miongoni mwa mambo mengine, kuhusu uvunjwaji  wa haki za binadamu nchini na dosari za uandikishaji wapiga kura.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI