BONGO MOVIES KIINGEREZA NI JANGA





Haya ni maoni ya mwanasheria kijana, Alberto Msando kuhusu makosa ya uandishi wa lugha ya kingereza kwenye kasha la filamu ya Mzee wa Swaga, iliyotengenezwa na kampuni ya Jerusalem, inayomilikiwa na msanii nguli wa filamu, Jacob Stephen 'JB '.
Alberto aliandika haya mara baada ya kubandika picha hiyo ya kwenye kasha :
“Bado ni marafiki zangu tu. Ninachotaka ni sanaa yenu ipendwe na watanzania waithamini. Soko la ndani ni kubwa sana. Ila endapo tu mtazingatia ubora. 
"Najua mtaji wa kuwekeza kwenye filamu ni kazi kuupata. Basi hayo makubwa tuyaache. Tubaki na haya madogo ambayo yako ndani ya uwezo wenu. 
"Hakuna from produced of shikamoo mzee. Na hakuna enterianments. Kiswahili ni sawa pia kutumia. Kwani ingeandikwa 

'Imeandaliwa na' kuna shida? 
"Na hakuna auto correct ya entertainment? UTASIKIA utetezi wa kitoto; sio lugha yetu!! Au ni bahati mbaya!”-Alberto alimalizia


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI