MCHEZAJI WA NIGERIA ALIYEFUNGA BAO KWA KUFANYIWA TAMBIKO

2013 Orange AFCON: Ivory Coast v Nigeria
Mshambuliaji wa Nigeria Emmanuel Emenike hivi karibuni aliifungia klabu yake bao lake la kwanza ikiwa imepita miezi mitatu alipofunga mara ya mwisho katika ligi ya Uturuki ambako anachezea klabu ya Fenerbace.
Emenike alifunga moja kati ya mabao mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya timu yaKarabuscorp na lilikuwa ni bao muhimu kwake kwani alikuwa hajafunga bao lolote kwa muda wa miezi mitatu.
Cha kufurahisha ni kwamba mshambuliaji huyu alifikia hatua ya kuamini kuwa hafungi kwa sababu amerogwa hali ambayo ilimfanya atafute msaada wa kiimani ambao aliupata hivi karibuni.
Emenike alikuwa hajafunga bao kwa muda wa miezi mitatu .
Emenike.
Emenike alikwenda kwa matabibu wa kitamaduni huko Uturuki ambao walimfanyia tambiko maalum la kumuondolea mkosi na siku chache baada ya tambiko hilo jamaa alifunga bao la kwanza baada ya kupita miezi mitatu bila kufunga goli lolote.
Nyota huyu hata hivyo amekanusha taarifa hizi japo zimesambaa nchini Uturuki ambako kila mtu anafahamu kuwa alilazimika kwenda kusaka msaada wa waganga ili avunje ukame wa mabao.
Emenike anaingizwa kwenye orodha ndefu ya wachezaji waliowahi kukumbwa na visanga vya imani za kishirikina baada ya Emanuel Adebayor ambaye hivi karibuni alimshutumu mama yake mzazi kwa kumroga.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI