STEWART AWAZUIA MORAD , MWANTIKA



KOCHA Mkuu wa Azam, Stewart Hall, amezuia mpango wa kuwatema wachezaji wanaocheza nafasi ya beki wa kati, Said Morad na David Mwantika.
Morad tayari ameshapewa mkataba wa miaka miwili wakati Mwantika naye anatarajiwa kuongezewa muda jambo linalozima ndoto za klabu zilizokuwa zikiwanyemelea wachezaji hao zikiwamo Simba na Mwadui Shinyanga.
Kocha Hall alisema anajua umuhimu wa Morad na Mwantika kwenye timu yake ndiyo maana ameamua wabaki.
Akielezea sifa za kila mmoja wao, alisema Morad ana nguvu, mbabe na ana uwezo wa kucheza mpira katika uwanja wenye mazingira yoyote vikiwamo vile vibovu vya mikoani.
Kuhusu Mwantika, alisema naye ni hivyo hivyo lakini zaidi ni beki wa kati mwenye kasi anayeweza kuwadhibiti washambuliaji machachari kama Mrisho Ngassa au Simon Msuva.
Akizungumza na Mwanaspoti, kocha huyo aliongeza: “Siwezi kuwaacha Morad wala Mwantika kwa sababu bado nawahitaji kikosini, kila mmoja wao ana umuhimu wake kwenye timu kama nilivyotaja sifa zao.”

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA