KIONGERA ARUDI RASMI SIMBA


                                               Raphael Kiongera

AMA kweli Simba imepania msimu ujao kwani imetangaza rasmi kumrejesha kikosini mchezaji wake kutoka Kenya, Raphael Kiongera, baada ya kuridhika na hali yake ya kiafya pamoja na uwezo wa uwanjani alioonyesha akiwa na KCB inayoshiriki Ligi Kuu Kenya (KPL).
Kiongera aliyepelekwa KCB kwa mkopo, ameshapona majeraha lake la goti na tayari ameanza kuonyesha makeke yake katika ligi hiyo ya Kenya akiwa amefunga mabao matatu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspope, alisema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakifuatilia maendeleo ya Kiongera hasa kwenye suala lake la afya na kwamba wameridhishwa na sasa wameamua kumrejesha Simba kwa ajili ya Ligi msimu ujao.
“Kiongera ni mchezaji halali wa Simba, tumejiridhisha kwamba amepona vizuri na ana uwezo mzuri wa kupambana uwanjani, hivyo tunatarajia kuwa atarejea na kujiunga na wenzake ifikapo kipindi cha maandalizi ya Ligi,” alisema Hanspope.
Kiongera aliumia goti la mguu wa kulia katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu msimu uliomalizika dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa Septemba 21, 2014 na kulazimika kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi minne.
Kurejeshwa kwa mchezaji huyo kunafanya idadi ya wachezaji wa kigeni kwa Simba kuwa wanne na kusaliwa na nafasi moja ambayo inayowaniwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo. 

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA