AZAM YAFUATA BEKI NIGERIA



AZAM inafanya usajili wa kimya kimya ambapo sasa inasaka beki mmoja katili aliyemaliza mkataba wake barani Ulaya, ili atue kwa matajiri hao wa Bara na Afrika Mashariki.
Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zinasema mabosi wa klabu hiyo wapo katika hatua za mwisho katika kumshusha beki mmoja ambaye jina lake limekuwa kificho kwa sasa.
Bosi huyo alisema beki huyo raia wa Nigeria atakuja nchini wakati wowote kuanzia wiki ijayo kuja kukamilisha usajili wake huo, huku pia wakiendelea kusaka saini ya mshambuliaji Mohamed Traore anayekipiga El Merreikh ya Sudan.
Usajili wa Traore ambaye ameonekana kuwavutia zaidi mabosi wa juu wa klabu hiyo, utakamilika tu endapo El Merreikh watapata mbadala wake ambapo klabu hiyo imemwambia itamuachia kama hilo litakamilika.
“Tunamleta huyo beki ingawa kwa sasa hatuwezi kukutajia jina, lakini ni raia wa Nigeria alikuwa anacheza soka Ulaya atakuja kuchukua nafasi ya Mwantika,” alisema bosi huyo. Mwantika anatajwa kutaka kutua Simba baada ya kumaliza mkataba wake na Wanalambalamba hao. 

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA