HANS POPPE: MASHABIKI SUBIRINI BONGE LA KOCHA


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe


MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe, amewaambia mashabiki na wanachama wa klabu hiyo akisema: “Tunaleta bonge la kocha nyie tulieni, msiwe na papara.”
Kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Simba, amesisitiza kwamba hawapo katika shinikizo lolote la kutangaza kocha kwa sasa kwani wanafanya mambo yao kwa umakini ili kumpata kocha wa maana.
Ingawa amekuwa mgumu kuweka wazi majina, alikiri kwamba wameshafanya mchujo na wanaye mtu ambaye wapo naye kwenye hatua za mwisho. Mwanaspoti linajua kwamba mchakato wa kumpata kocha wa zamani wa Taifa Stars, Kim Poulsen, umegonga mwamba na sasa wamegeukia upande mwingine ambapo imeelezwa wameanza kumsaka kocha raia wa Ufaransa, Didier Gomez de Roza ambaye pia bado hawajafikia makubaliano ya mwisho.
Didier amewahi kufanya kazi na Rayon ya Rwanda na hivi karibuni alikuwa Cameroon. Lakini wapo vigogo wa Simba ambayo wanashawishi Mserbia,Goran Kopunovic arudishwe huku wengine wakitaka aletwe kocha wao wa zamani, Milovan Cirkovic.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA