Posts

Showing posts from June, 2015

MH. SUGU AUDANGANYA UMMA, FAIZA AFUNGUKA

Image
Faiza Ally afunguka mh Sugu ni mwongo hawajahi kutoa laki tano matumizi ya mtoto kila mwezi kama alivyodai bungeni.26 june mbunge huyo alidai amekua akilipia ada ya mtoto milioni tatu,televisheni ya katuni na matumizi madodogo madogo.Katika utetezi huo alimbibi hadi kutoa mchachozi hadharani baada ya mbunge Martha wa viti maalum kumshutumu ana nyanyasa wanawake.                                                              chanzo nipashe june 28.

MWALIMU ANYOLEWA SEHEMU ZA SIRI KISHIRIKINA

Image
WALIMU katika shule ya msingi  Nambaza Kata ya Nansimo wilayani Bunda,    wamesema watahama shule hiyo endapo serikali ya wilaya hiyo haitachukua hatua madhubuti kukomesha ushirikina shuleni hapo. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Sospiter Mafuru,  alisema walimu wake wanafanyiwa vitendo vya ushirikina ikiwa  ni pamoja na kusumbuliwa   usiku  na kunyolewa  nywele   sehemu za siri. Alitaja vitendo vingine kuwa ni kuvuruga vyombo vya ndani wakati wa usiku, kumwaga michuzi na damu kwenye mashuka na nguo za walimu hao. “ Vitendo hivi vimetishia usalama wa walimu hadi sasa walimu watatu wa kike wamehama shule hii kwa hiyo tunaomba jamii ya Nambaza wachukue hatua,” alisema. Alisema awali   ushirikiana huo ulianza kwa wanafunzi  kuugua na kuanguka ovyo na baadaye kwa walimu na aliomba Serikali   kuchukua hatua na kukaa na wananchi wao. Mafuru alisema hadi sasa ana    walimu ti...

WEMA SEPETU AMTAJA ANAYEMZUIA KUPATA MTOTO

Image
Ishu ya  Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutopata ujauzito imeshazungumzwa mara kadhaa na hata yeye mwenyewe alishawahi kujitokeza na kuizungumzia lakini safari hii amelizungumzia kwa njia tofauti.  Wema ambaye pia ni muigizaji wa filamu, awali alisema sababu kubwa ya kutopata ujauzito ni masuala ya kiafya lakini safari hii ametoa kauli tata ambayo inahusiana na imani za nguvu za giza.   Wema ambaye alifunguka hayo hivi karibuni, anadai kuwa yawezekana marehemu Steven Kanumba anahusika kwenye suala hilo.   Mizimu ya Kanumba “Unajua hili suala la mtoto linanisumbua sana yaani na linaniuma kwa sababu napenda watoto sana na pia napenda kuitwa mama, nimehangaika sana katika kuhakikisha nafanikiwa katika hili lakini ndiyo hivyo imeshindikana.   “Serious! Ilifika kipindi yaani nilikuwa nachukia nilipokuwa nikiziona siku zangu, nilikuwa sipendi kukutana na hiyo hali kwa sababu naumia sana lakini ndiyo hivyo baada ya kuhangaika sana inabidi nimwachie M...

SUGU ATOA MACHOZI BUNGENI KUHUSU MWANAYE, NAIBU SPIKA ADAI MJADALA UFUNGWE KULINDA HAKI ZA MTOTO

Image
               Sugu na mwanaye Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amejikuta akiangua kilio bungeni baada ya kutoa hoja binafsi kumjibu Mbunge wa viti maalum wa Singida ‘CCM’ Martha Mlata, aliyemshutumu kwa kumpora mtoto wake wa kike Sasha kutoka kwa mzazi mwenzake Faiza Ally. Akijibu tuhuma za Mlata, Sugu alisema kuwa ameumizwa na kusitikishwa kwa suala la kifamilia kuingizwa ndani ya bunge na kuomba kuheshimiwa kwa kuwa masuala yale ni masuala binafsi. “Asante sana Naibu Spika, naomba nitoe maelezo binafsi, tarehe 25 June 2015, Mbunge Martha Mlata alidai kuwa kuna Mbunge wa CHADEMA amempora mwanamke mmoja mtoto mdogo wa miaka miwili na amempora wakati Mbunge huyo amekuwa hatoi matunzo kwa mama yake… Mlata aliwataka Wabunge wote wanawake kuungana kukemea kitendo alichodai kimefanywa na Mbunge huyo,"  Alisema  Sugu  na  Kuongeza: “Hakutaja jina la Mbunge aliyemhusisha na madai yake ila alidai kuwa ni msa...

SAKATA LA FAIZA ALLY KUNYANG'ANYWA MTOTO NA SUGU LATUA BUNGENI

Image
Siku chache zimepita tangu hukumu ya kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kutolewa dhidi ya mzazi mwenzake Faiza Ally,baada ya kuiomba mahakama kumchukua mtoto wao, hali iiyopelekea mahakama kutoa hukumu kuwa mtoto achukuliwe na Mbunge huyo,  jambo lililofanya sakata hilo kutinga bungeni.   Baadhi ya wabunge na wadau mbalimbali wamedai kuwa mtoto bado ni mdogo sana kuweza kuishi na baba yake na kutoa maoni kuwa mtoto arudishwe kwa mama yake kwa kuwa kila mtu ana mapungufu na kusema kuwa mtoto bado ana haki ya kuwa karibu na mama yake.   Kwa mujibu wa Mbunge Martha Mlata jana  alisema kuwa;  “Tuna Mbunge mwenzetu amemnyanyasa mwanamke mwenzetu ametumia siku moja Mahakamani kumnyang’anya mtoto wa miaka miwili.. Mbunge huyu anajijua kwa sababu mwanamke huyo anaitwa Faiza.. Faiza arudishiwe mtoto wake”.    Hoja hiyo ikachangiwa na Mbunge David Kafulila alisema  “Hii nchi ina mihimili mitatu, Bung...

FISI AMNYANG'ANYA MAMA MTOTO NA KUMLA, ABAKISHA KICHWA NA UTUMBO

Image
Watoto wawili wenye umri wa kati ya miaka miwili na mitano wameuawa na fisi katika Kijiji cha Mnkola, Kata ya Ibihwa wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma katika matukio mawili tofauti.    Mwenyekiti wa Kitongoji cha Teya Kata ya Ilindi wilayani hapa, Paul Mwaja alisema kuwa watoto hao wameuawa katika matukio mawili ndani ya kipindi cha wiki moja.   Mwaja alisema tukio la kwanza lilitokea juzi ambapo mtoto mmoja wa kiume mwenye aliuawa na fisi wakati akiwa na wenzie wawili wamelala.     “Alikwenda fisi katika eneo hilo na kumvuta (mtoto mmoja) na kumtafuna hadi akamuua,” alisema Mwaja.   Alisema usiku wa kuamkia jana, fisi huyo alirudi tena katika kijiji hicho na kumnyang’anya mama mmoja mtoto wake mdogo mwenye umri wa miaka miwili.   Mwaja alisema fisi huyo alimla mtoto huyo na kumbakisha kichwa na utumbo tu, hali iliyozua taharuki katika kijiji hicho.   Hata hivyo, alisema baada ya tukio hilo wananchi waliamua kufanya msako na kumka...

STEWART AWAZUIA MORAD , MWANTIKA

Image
KOCHA Mkuu wa Azam, Stewart Hall, amezuia mpango wa kuwatema wachezaji wanaocheza nafasi ya beki wa kati, Said Morad na David Mwantika. Morad tayari ameshapewa mkataba wa miaka miwili wakati Mwantika naye anatarajiwa kuongezewa muda jambo linalozima ndoto za klabu zilizokuwa zikiwanyemelea wachezaji hao zikiwamo Simba na Mwadui Shinyanga. Kocha Hall alisema anajua umuhimu wa Morad na Mwantika kwenye timu yake ndiyo maana ameamua wabaki. Akielezea sifa za kila mmoja wao, alisema Morad ana nguvu, mbabe na ana uwezo wa kucheza mpira katika uwanja wenye mazingira yoyote vikiwamo vile vibovu vya mikoani. Kuhusu Mwantika, alisema naye ni hivyo hivyo lakini zaidi ni beki wa kati mwenye kasi anayeweza kuwadhibiti washambuliaji machachari kama Mrisho Ngassa au Simon Msuva. Akizungumza na Mwanaspoti, kocha huyo aliongeza: “Siwezi kuwaacha Morad wala Mwantika kwa sababu bado nawahitaji kikosini, kila mmoja wao ana umuhimu wake kwenye timu kama nilivyotaja sifa zao.”...

MKWASA AANZA YAKE TAIFA STARS

Image
KOCHA Mkuu mpya wa Taifa Stars, Boniface Mkwasa, ameanza yake baada ya kutangaza benchi lake la ufundi sambamba na kikosi kipya cha timu hiyo akiwajumuisha kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ na Samuel Kamuntu ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa mchezaji huyo wa JKT Ruvu kuitwa Stars. Mkwasa alitangaza jopo lake jipya jana Jumatano ambalo linawajumuisha Juma Mgunda, Abdallah Kibadeni, Hemed Morocco na Peter Manyika. Mgunda ameteuliwa kuwa Meneja wa timu hiyo, huku Manyika akiwa ni Kocha wa Makipa wakati Morocco anakuwa Kocha Msaidizi na Kibadeni ni Mshauri wa timu na mtunza vifaa ni Hussein Sued ‘Gaga’ ambapo Mratibu wa timu hiyo anakuwa Ahmed Mgoyi. Juu ya kikosi kipya cha timu hiyo kinachojiandaa na pambano la marudiano dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ kuwania tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezani wa Ndani (Chan) 2016, Mkwasa ameita jumla ya wachezaji 26 ambao ni pamoja na makipa ‘Barthez’ (Yanga), Mwadini Ali (Azam), Mudathir Hamis (KMKM). Wengine ni mab...

PROFESA MUHONGO AUMBUKA CCM MAKAO MAKUU

Image
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Waziri aliyejiuzulu kutokana na kashfa ya uchotwaji wa mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, Profesa Sospeter Muhongo, jana aliumbuka  baada ya Chama chake kukataa kupokea lundo la makasha ya CD (santuri) zenye picha za wadhamini wake 675. Badala yake, alielezwa kwamba, hakuna kipengele kinachoruhusu kuwa na kumbukumbu hiyo. Profesa Muhongo, alirejesha fomu yake ya kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, saa 9:57 asubuhi na kumkabidhi Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) na Oganaizesheni, Mohamed Seif Khatibu kwenye makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma. Baada ya kukabidhi fomu za wadhamini wake katika mikoa 15 aliyopita, Profesa Muhongo alitoa pia makasha 15 yenye CD za picha ambazo alidai amefanya hivyo ili kuonyesha hajapita njia ya mkato akidai anaamini mtu sahihi atakayeweza kuwavusha watanzania kwa sasa, ni yeye na si mgombea mwingine kati ya makada wote...

AJINYONGA BAADA YA KUGUNDULIKA KUWA ANAVIRUSI VYA UKIMWI

Image
MKAZI mmoja wa Mtaa Myegeya katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, Mathias Ngimba (41), amekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga  kwa kutumia kipande cha nguo kwa kile kilichodaiwa baada ya kupimwa afya yake alibainika kuwa ana maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi  (VVU).   Akizungumza jana Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela,  alisema tukio hilo limetokea Juni 20, mwaka huu saa 4 asubuhi katika nyumba ambayo aliwekwa na kaka yake marehemu aitwaye Festo Ngimba.   Kamanda alisema marehemu Mathias Ngimba, inadaiwa alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya kichwa pamoja na tumbo la kuhara ndipo alipochukua maamuzi ya kwenda katika Zahanati ya jeshi iliyopo Chaburuma  na kupimwa afya yake ili kubaini tatizo linalomsumbua.   “Marehemu alipofika zahanati alipimwa na kubainika maradhi yanayomsumbua aligundulika kuwa ameshapata maambukizi ya VVU ndipo akarejea nyumbani alipokuwa akiishi na kuamua kuchukua maamuzi wa kujinyonga kwa kutu...

AFYA YAKO:AFYA YA NGOZI (Sehemu Ya Kwanza).

Image
Na Dr. Richard Zuberi UTANGULIZI Tunamshukuru Mungu kwa nafasi nyingine ambayo ametupa kuwepo hai tena na hata kuweza kushiriki darasa letu fupi hapa, pia napenda nimshukuru kila mmoja ambaye amekuwa akishiriki katika meza yetu hapa kwa namna moja ama nyingine, hata kwa kusoma tu na kupita, kufanya kwako hivyo kunanisukuma kuendelea kusema yale machache ambayo kwa sehemu ninayafahamu. Wiki hii tutaanza kuangalia somo la AFYA YA NGOZI, soma kwa faida yako na jirani yako, soma hata kama una allergy (mzio) na maandishi/maandiko. Ngozi sio kiungo kigeni au kilichojificha kama ulivyo moyo, figo au maini, ngozi ipo nje na kila mtu anaweza kuiona. Ngozi ndiyo kiungo kikubwa kuliko viungo vyote katika mwili wa mwanadamu, ngozi imegawanyika katika sehemu kubwa tatu; ngozi ya nje, ya kati nay a ndani. KAZI ZA NGOZI Kulinda mwili mbali na maambukizi ya wadudu wasababishao magonjwa,Kulinda mwili usipoteze maji kama mvuke,Kulinda sehemu za ndani ya mwili zisipate jereha hasa pale ngozi i...

CCM YABARIKI UBUNGE WA WEMA SEPETU

Image
Siku chache baada ya mwanadada anayefanya vizuri kwenye filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kutangaza nia ya kugombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), chama hicho kimempa baraka mrembo huyo kwa uamuzi wake huo. Akizungumza na mtandao huu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi wowote ule ilimradi awe mwanachama hai, hivyo kwa Wema kugombea ubunge wa viti maalum ni haki yake na amefanya uamuzi sahihi.   “Kugombea uongozi ni haki ya kila mwanachama, Wema ana haki, kwanza ni mwanachama hai na baba yake alikuwa mwanachama mzuri sana wa CCM mpaka anafariki dunia, hivyo chama chetu huwa hakikutani na watu barabarani tu, bali wanakuwa ni halali kabisa mpaka wanatangaza kugombea,”  alisema Nape.   Hata hivyo, alisema wasanii wote waliotangaza kugombea kupitia chama hicho hawajakurupuka bali ni wanachama hai na wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali za kichama, tangu kwenye kampeni za ...

MKULIMA MSAKA URAISI ATUA MOROGORO KUTAFUTA WADHAMINI

Image
MKULIMA wa Kigoma anayewania kupitishwa na CCM agombee urais kwa chama hicho, Idelphonce Bilole, ametua mkoani Morogoro akiendelea kutafuta wadhamini katika mikoa 15 nchini, huku akisisitiza elimu si kigezo cha yeye kushindwa kuwania nafasi hiyo ya juu.   Bilole aliyasema hayo jana katika ofisi ya CCM Wilaya ya Morogoro ambapo alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kiongozi ni lazima ajue kusoma na kuandika na kwamba CCM ni chama pekee ambacho hakina ubaguzi.   Aidha, alisema mwaka 2003 alifuatwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho wakimtaka ajiandae ili aweze kuwania nafasi hiyo kwa mwaka 2005 ambapo alisema alikubali na aliandika barua ya kuomba kuteuliwa, lakini kutokana na sababu ambazo yeye hakuzifahamu barua ile ilichelewa na hivyo kuamua kuvuta subira.   Hata hivyo alisema kuwa mwaka huu ameona ni muda muafaka wa yeye kuwania nafasi hiyo ambayo wanachama wenzake wamekuwa wakimuomba kugombea ambapo alisema kuwa ameshafika katik...

MJAMZITO AJIFUNGULIA BAFUNI DAKIKA CHACHE BAADA YA WAUGUZI KUMFUKUZA

Image
MJAMZITO aliyefahamika kwa jina la Rotha Bujiku, amejifungulia bafuni karibu na zahanati ya kijiji baada ya kudaiwa kufukuzwa na wauguzi waliokuwa zamu siku hiyo, kwa maelezo kuwa anajifungua kila mwaka.   Tukio hilo lilitokea wilaya ya Maswa katika mkoa wa Simiyu majira ya saa 2 asubuhi baada ya mjamzito huyo kufika katika zahanati hiyo kwa lengo la kupata huduma ya kujifungulia kwa wataalamu.   Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililovuta umati wa watu, mjamzito huyo alikataliwa kupokewa na muuguzi wa zamu aliyetajwa kwa jina la Constansia John.   Ilielezwa kuwa muuguzi huyo alikataa kumpokea kwa madai kuwa mjamzito huyo alishapewa maelekezo tangu awali kuwa anatakiwa akajifungue katika hospitali ya wilaya ya Maswa kwani amekuwa akizaa watoto kwa mfululizo.   Inaelezwa kwamba, wakati Rotha akiugulia maumivu ya uchungu, muuguzi huyo alimpigia simu ya mkononi Muuguzi Mkunga wa zahanati hiyo, Leticia Kachumi kumjulisha hali hiyo na alipofika a...

TANZIA: MBUNGE WA GEITA AFARIKI DUNIA

Image
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Geita (CCM) Mheshimiwa Donald Kevin Max (58) amefariki dunia. Kufuatia taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda (Mb) kwa Waheshimiwa Wabunge wote pamoja na umma kwa ujumla, Mhe. Max amefariki dunia tarehe 23 Juni, 2015 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu. Kwa mujibu wa taarifa hii, taarifa zaidi juu ya msiba huu zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia kadri zitakavyopatikana ikiwa ni pamoja na ratiba ya Mazishi. “BWANA ametoa, BWANA ametwaa, Jina la BWANA lihimidiwe.” Amina. Imetolewa na: Ofisi ya Bunge, Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa, DODOMA

IJUE AFYA YAKO: HATARI YA KUTONYONYESHA

Image
Na Dk. Richard Zuberi Mimi niliye mdogo kwenu nimeona vema sana kwamba kila Jumatano kwa kadri Mungu atakavyotuwezesha tutakuwa pamoja katika darasa huru lenye kichwa “MEZANI KWA TABIBU”. Yale tutakayoshirikishana hapa katika meza hii sio FACT yote kabisa, kila siku kuna tafiti mpya zinafanywa na matokeo na maarifa mapya yanapatikana kwa hiyo uwe huru kuchukua cha kukufaa na kuacha kisichokufaa. Jumatano hii ya kwanza, tutaangalia kwa sehemu tu hatari ya kutonyonyesha mtoto. Katika jamii yetu sasa kuna maendeleo makubwa sana tumeyapata ikiwa ni pamoja na mama zetu wa sasa kuwa na majukumu makubwa ya kutafuta fedha zaidi ya kulea watoto/familia na wakati mwingine kushindwa kunyonyesha watoto wao. Lakini pia kuna kundi la wamama wa kisasa ambao wameamua tu kwamba hawataki kunyonyesha kwa sababu tu za kuogopa kupoteza muonekano wao wa nje hasa matiti kupoteza shape nzuri. Wakati mwingine tumeona tu kwamba kwa kuwa kuna maziwa ya viwandani ambayo yanapatikana na kwa kuwa tuna...

BEKI WA ZAMANI AWAPA SOMO WENZAKE BONGO

Image
Aliyekuwa beki wa Simba, David Naftal  BEKI wa zamani wa Simba, David Naftal anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Ushuru ya Kenya, amewaambia wachezaji wenzake nchini ambao wanakosa nafasi kwenye timu zao hasa Simba na Yanga kuiga mfano wa Dan Sserunkuma. Dan alisajiwa Simba wakati wa usajili wa dirisha dogo akitokea Gor Mahia ya Kenya akiwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Kenya (KLP) lakini alishindwa kutamba ndani ya Simba ambapo aliondoka akiwa amefunga mabao matatu pekee huku akipotezewa na kocha Goran Kopunovic. Sasa Naftali aliwapa akili wachezaji wa Kibongo kwa kuwaambia  kwamba wachezaji wengi ndani ya Simba na Yanga hawapati nafasi za kucheza na wanaogopa kuziacha timu hizo kutokana tu na ukubwa wa majina ya timu husika pasipo kujali kushuka kwa viwango vyao. “Ni kweli katika nchi za Afrika Mashariki, Tanzania ndiyo inayolipa vizuri lakini je usipocheza hiyo pesa unaitoa wapi, maana najua timu za Simba na Yanga ukicheza ndio maisha yako yanakuwa mazu...

STRAIKA MPYA SIMBA NI NOMA

Image
                                      Straika Laudit Mavugo  SIMBA achana nao kabisa, kwani wamefanya kitu ambacho hakuna aliyetarajia katika usajili wao wa msimu ujao. Klabu hiyo iliamua kumfungia safari straika mkali wa Vital’O mpaka Burundi na kisha kumsainisha. Straika huyo, Laudit Mavugo amesaini mkataba wa miaka miwili. Na kama ulikuwa hujui ni kuwa mchezaji huyo amesajiliwa kwa kitita cha Dola za Kimarekani 20 elfu na mshahara wa Dola 1,000 ambazo ni kama Sh. 2.2 Milioni. Dau alilosajiliwa na mabosi wa Msimbazi limeongeza thamani ya mchezaji huyo kinara wa mabao wa Ligi ya Burundi kwani kabla ya hapo alikuwa akiichezea Vital’O kwa dau linalokadiriwa Sh. 4 Milioni na mshahara wa Sh. 400,000 tu. Hujakosea ni Laki Nne tu! Inaelezwa kuwa mabosi wa Simba waliamua kutoboka kiasi hicho cha fedha kutokana na kukubali ukali wa Mavugo ambaye wanaamini akiungana na Mussa Mgo...