ROBERT HUTH: BEKI WA STOKE CITY ALIYEUSHANGAZA ULIMWENGU KWA KUICHUKIA CHRISTMAS

Beki raia wa Ujerumani anayecheza kwenye klabu ya Stoke City Robert Huth hali imekuwa tofauti baada ya mchezaji huyo kuonyesha hisia za kinyume kabisa na wachezaji wengine .
Mchezaji huyu aliustaajabisha ulimwengu kwa kitendo chake cha ku-tweet hisia zake kuhusiana na sikukuu hii ambayo inadhimishwa ulimwenguni kote.

Tweet inayoonyesha hisia za beki Robert Huth kwa sikukuu ya Christmas.

Robert Huth kwa kutumia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter aliandika kuwa anaichukia krismasi na hakutoa sababui za msingi za chuki aliyo nayo kwa sikukuu hii .
Hakuna aliyeweza kufahamu chanzo hasa cha utofauti huu toka kwa beki huyu Mjerumani ambaye amejijengea sifa kama beki mgumu asiyetetereshwa na washambuliaji awapo uwanjani .

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI