ALIYEWAKOSOA WATOTO WA OBAMA AJIUZULU

                        Watoto wa Obama wakiwa na mama yao
New York, MArekani. Wakati watanzania wametajwa kuhusika na kashfa ya wizi wa sh 306 bilioni katikaakaunti ya Tegeta escrow wakigoma kujiuzulu, mfanyakazi wa Repiblican,Elizabeth Lauten amejiuzulu baada ya kuwakosoa watoto wa rais Barack Obama.
Elizabeth Lauten ambaye ni Ofisa Mkuu wa Mawasiliano wa mwanasiasa mkuu wa chama hicho, Stephen Fincher,alijiuzulu jana baada yab kushambuliwa na watu kadhaa kwa kuwakosoa watoto hao kwa kuvaa nguo fupi wakati wa hafla ya jioni iliyofanyika ikulu, Marekani.
Lauten aliwataka watoto hao kuwa makini wanapokuwa katika matukio ambayo jamii inawatazama kupitia vyombo vya habari.
Lauten, aliwakosoa Sasha na Malia kwenye ukurasa wake wa Facebook, lakini baada ya muda mfupi kupita alifuta ujimbe huo kutokana na watuwengi kumshambulia.
Akiomba radhi Lauten alisema baada ya kutafakari aligundua kwamba hata yeye wakati mtoto hakupenda kukosolewa.
"Baada ya maombi ya saa kadhaa ambayo yalifanywa na wazazi wangu na kurudia kuusoma ujumbe niliouandika nilibaini kuwa ujumbe huo haukuwa sawa, hivyo naomba radhi kwa usumbufu niliousababisha", alisema mkurugenzi huyo.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI