DUDE: WASANII WENGI WA BONGO WANA UKIMWI


                   Kulwa Kikumba ''Dude''

Staa wa Fialmu za kibongo Kulwa Kikumba ''DUDE'' amesema kuelekea mwisho wa mwaka wasanii wengi wana UKIMWI na mbaya zaidi wanaambukizana wao kwa wao.
 Dude amesema mastaa wazima wanahesabika na kutaja sababu kuwa ni kuibiana na kubadilishana wapenzi bila woga.

Utakuta Mbongo Fleva ana mtu kwenye Bongo Muvi na Mbongo Muvi ana mtu kwenye dansi au kwa mamis au hata wacheza mpira, ukitaka kuujua ukweli tangaza dau kuwapima mastaa uone watakaojitokeza,” alisema Dude.
Aidha, Dude alisema anavyoona yeye ingeanzishwa kampeni ya mastaa wa Bongo kupima Ukimwi kwani anawahofia watoto wa kizazi kipya zaidi ambao wanajikuta wanaingia pabaya na kuzima ndoto zao. 

Chanzo Gazeti la Ijumaa


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI