PHIRI:AKITOKA MKUDE ANAINGIA AWADH


             Kocha Patrick Phiri 

KOCHA wa Simba, Patrick Phiri, amepiga hesabu za mbali na kusema kiungo wake Awadh Juma anaweza kabisa kucheza nafasi ya Jonas Mkude ikitokea dharura katika mchezo dhidi ya Yanga wa Nani Mtani Jembe wa Desemba 13.
Simba na Yanga sasa zipo katika mazoezi makali kujiandaa na mechi hiyo itakayojumuisha wachezaji wengi wapya, lakini Simba itaingia na kumbukumbu nzuri kwani mwaka jana kwenye mechi kama hiyo ilishinda mabao 3-1.
Kwa muda mrefu Simba imekuwa ikionekana kumtegemea zaidi Mkude katika nafasi ya kiungo na kuonekana ndiye pekee anayemudu nafasi hiyo.
Hata hivyo Phiri amesema: “Kama unakumbuka katika mechi dhidi ya Yanga, Mkude aliumia na nikamchezesha Awadh Juma katika nafasi yake na hakuna kilichotokea kwani hatukuweza kuruhusu bao, hivyo huyu (Awadh) ni chaguo sahihi la kuwa mbadala wa Mkude.
“Hata katika mechi dhidi ya Yanga (Desemba 13), ikitokea Mkude amepata matatizo Awadh atacheza nafasi yake bila matatizo, hivyo wana Simba wasiwe na wasiwasi na kudhani tunamtegemea mchezaji mmoja tu, hapana.”
Hata hivyo Mkude aliyeongezewa mkataba wake na Simba hivi karibuni, ana hali nzuri na anafanya mazoezi na wenzake kujiandaa na mechi ya hiyo sambamba na mechi za Ligi Kuu Bara zitakazoendelea.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI