IVO, MASHABIKI BIFU ZITO

                        Kipa wa Simba, Ivo Mapunda.

NI bifu! Ndiyo unavyoweza kusema baada ya mashabiki   wa Simba kumshushia lawama za moja kwa moja kipa wao namba moja, Ivo Mapunda kutokana na kipigo cha bao cha 1-0, walichopata kutoka kwa Kagera Sugar.
Mchezo huo wa raundi ya nane, ulipigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Baada ya mchezo huo, mashabiki walitoa lawama kwa Mapunda kuwa ndiye aliyechangia kufungisha bao hilo kutokana na kutokuwa makini langoni.
“Wewe angalia mpira wa kurushwa baada ya kuupiga ngumi anataka kuudaka, kama siyo uzembe ni nini,” alisikika shabiki mmoja akilalamika.“Huyu Mapunda siku zote hawezi kucheza mipira ya krosi na hata bao lile limedhihirisha hilo, nashangaa kwa nini mpaka sasa ameshindwa kubadilika, bao lile ni uzembe wake,” alisikika shabiki mwingine.
Lakini wakati mashabiki wakisema hivyo, kocha wa timu hiyo, Patrick Phiri alitoa lawama zake kwa washambuliaji wake kwa madai kuwa walishindwa kutumia nafasi nyingi walizopata.“Tumefungwa bao la kimichezo sina haja ya kutoa lawama kwa mtu, lakini safu ya ushambuliaji haikuwa makini na imepoteza nafasi nyingi za wazi,” alisema Phiri.
Katika hatua nyingine, viongozi wa timu hiyo hawakuonekana katika vyumba vya kubadilishia nguo kama ilivyo kawaida yao baada ya timu yao kupoteza mchezo huo.Mara nyingi kila wanapopata ushindi baadhi ya viongozi hao hujumuika pamoja na wachezaji wao vyumbani lakini jana hali ilikuwa tofauti.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI