TUNDU LISSU ASHAMBULIWA NA WANANCHI BAADA YA KUTANGAZA MAANDAMANO NCHI NZIMA




Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ndugu Tundu Lissu amekiona Cha Moto Baada ya Kutangaza maandamano siku ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa 10 mwaka huu, na hiyo ni kama Serikali kupitia Tume huru Ya Uchaguzi itachishidwa Kuweka utaratibu sawa kuelekea uchaguzi huo.

Wananchi ambao wametoa maoni Yao wameonesha kuchukizwa na kauli ya Tundu Lissu ya Kutaka wananchi kuandamana Nchi nzima wakati uchuguzi ukiendelea, wengi wao wakiamini kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa Raia na Mali zao.



Itakumbukwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu aliweka bayana na kusema kuwa siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu, chama hicho kitaitisha maandamano ya kuuzuia uchaguzi usifanyike.

Kauli hiyo ya Lissu, inajibu swali kuhusu mbinu ambayo chama hicho itaitumia kuzuia uchaguzi kuendana na ajenda yake ya ‘No Reforms, No Election’ (bila mabadiliko, hakuna uchaguzi).

Kauli ambao kwa wanachadema wanaona ni rafiki na nzuri lakini kwa CCM na wale wasio na mlengo wowote wakichama wakiona kama huwenda ikaenda kuibua Vurugu na uvunjifu wa amani.
Lissu amesema hayo Jana , Jumatatu Aprili 7, 2025 wakati akihutubia mkutano wa hadhara Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara katika ziara ya kutoa elimu kuhusu ‘No Reforms, No Election.’

Amesema iwapo Serikali haitafanya mabadiliko ya sheria na kanuni za uchaguzi, chama hicho kitawahamasisha wananchi kuandamana kuuzuia uchaguzi usifanyike.

Ambapo alisema kwamba :“Hatutaenda kupiga kura, hatutaenda kujiandikisha, siku ya kupiga kura tutaandamana, watatufunga wote? Kuna sheria ya Tanzania inayosema lazima tushiriki kwenye chaguzi za kijinga?” amehoji Tundu Lissu ":.

Hii ni mwendelezo wa Magongano wa matamshi kati ya vyama viwili vikibwa vya kisiasa hapa Nchini.

Nini mtazamo wako kuelekea katika uchaguzi Mkuu wa mwezi wa 10 mwaka huu.






Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA