CHAMA IKATAA YANGA MOJA KWA MOJA
Mchezaji mahiri wa Young Africans, Clatous Chama, ameibua gumzo lingine kwenye mitandao ya kijamii. Inaripotiwa kuwa kiungo huyo fundi amefuta (unfollow) akaunti rasmi ya klabu yake ya Young Africans kwenye mtandao wa Instagram. Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba, Chama ameanza tena kuifuatilia (follow) akaunti ya klabu yake ya zamani, Simba SC, ambayo aliifuta alipojiunga na Yanga.
Kitendo hiki kimeacha maswali mengi kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania. Je, hii ina maana gani? Kuna nini kinachoendelea nyuma ya pazia? Wengi wanasubiri kwa hamu kujua hatima ya kiungo huyo mwenye uwezo wa kubadilisha mchezo.
Hii si mara ya kwanza kwa Chama kufanya vitendo vinavyozua uvumi kuhusu uhamisho wake. Mashabiki wanasubiri kwa shauku kujua kama huu ni mwanzo wa kurejea kwake Simba SC au ni mchezo mwingine wa akili kwenye ulimwengu wa soka.
Kwa upande wa baadhi ya mashabiki walidai kuwa, Kiungo huyo kutoka Zambia tayari yupo katika harakati za kuagana na wanajangwani kutokana na kukosa nafasi kwenye mechi za msimu huu.
Comments
Post a Comment