MICHEZO: RASMI SASA FEI TOTO KURUDI YANGA, AZIKOSA OFA HIZI
Katika hatua mpya ya kusisimua kwenye dirisha la usajili, klabu ya Yanga SC imeingia rasmi kwenye mazungumzo na kiungo wa Azam FC, Feisal Salum maarufu kama Fei Toto, kwa lengo la kumsajili tena na kumrejesha Jangwani.
Jioni ya jana, viongozi wa Yanga wamekutana na wawakilishi wa mchezaji huyo kuwasilisha pendekezo lao rasmi. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, ofa iliyotolewa na Yanga (hasa katika malipo ya awali ya usajili - sign-on fee) ni kubwa zaidi kuliko ile ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC.
Ikumbukwe kuwa Yanga inatarajia kumuuza nyota wao Aziz Ki mwishoni mwa msimu huu, huku mchezaji mwingine wa nafasi hiyo, Pacome, akiwa bado hajasaini mkataba mpya. Hii inawasukuma viongozi wa Yanga kumtazama Fei Toto kama chaguo mbadala lenye ubora.
Kwa sasa, Fei Toto anashikilia jumla ya ofa tatu kutoka ndani ya Tanzania:
1. Ofa ya mkataba mpya kutoka Azam FC.
2. Ofa ya usajili kutoka Simba SC.
3. Ofa kubwa (mega deal) kutoka Yanga SC.
Hata hivyo, kikwazo kikuu kinachoweza kuzuia kurejea kwake Yanga ni msimamo wa mama yake mzazi, ambaye bado hajaridhia uhamisho huo. Licha ya hilo, taarifa zinaonesha kuwa Yanga wapo tayari kuchukua hatua ya kuomba msamaha ili kufanikisha dili hilo.
Imeandikwa Hans Rafael - mtangazaji na mchambuzi wa michezo Crown FM
Comments
Post a Comment