CHADEMA YAFUNGIWA KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU OCTOBER 2025
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi – INEC Ramadhani Kailima amesema Chama cha Demokrasia na maendeleo - CHADEMA hakitoshiriki Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2025 na chaguzi zote ndogo kwa muda wa miaka mitano kufuatia kutosaini kanuni za maadili ya Uchaguzi.
Kailima amsema hayo mara baada ya zoezi la kusini kanuni za maadili ya Uchaguzi leo April 12, 2025 katika ofisi za Tume hiyo Njedengwa Jijini Dodoma ambapo vyama vya siasa 18 ndivyo vimesaini isipokuwa CHADEMA.
“Chama cha CHADEMA ambacho hakikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2025, hakitashiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.” Ramadhan Kailima mkurugenzi wa Tume huru ya Uchaguzi.
Mapema asubuhi hii, Katibu mkuu wa chama hicho alinukuliwa katika mitandao ya kijamii alisema:
"Katibu Mkuu CHADEMA sitakuwepo kwenye kikao cha tarehe 12 Aprili 2025 cha kushauriana na kusaini maadili ya uchaguzi ya 2025.
Ifahamike kuwa mwenye mamlaka ya kusaini maadili ya uchaguzi kwa niaba ya chama cha siasa ni Katibu Mkuu.
Katibu Mkuu sijateua kiongozi au afisa yoyote kwenda kushiriki kwa niaba yangu katika kikao hicho kitakachofanyika katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi".
"Katika ukurasa rasmi wa CHADEMA wa mtandao wa X wiki hii iliwekwa taarifa inayosema;
Taarifa za awali, waliokamatwa mpaka sasa.
1. Mhe. Tundu Lissu - Mwenyekiti wa Chama Taifa
. Mhe. Aden Mayala - Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini
3. Mhe. Felius Festo - Mratibu wa Uhamasishaji BAVICHA Taifa
4. Shija Shebeshi
5. Mlinzi
Kwa hatua ya sasa Tunalitaka jeshi la Polisi kuwaachia viongozi wetu Haraka na bila masharti yoyote."
Baada ya masaa machache ndipo mfululizo wa taarifa za chama hicho kutoka matamo mbalimbali yanayopatikana katika ukurasa wake wa wa X.
Chanzo: Millard Ayo & EATV
Comments
Post a Comment