MIKOA INAYOONGOZA KWA UCHAWI TANZANIA
Kumekuwa na Maswali mengi miongoni mwa watu, kuhusu mikoa inayosemekana kuwa na uchawi zaidi nchini Tanzania. Baada ya kufuatilia vyanzo mbali mbali vya habari, na kufanya mlinganisho na maoni ya watu, mikoa iliyotajwa kuwa na uchawi zaidi nchini Tanzania nikama ifuatayo;
Sumbawanga (Rukwa), Sumbawanga ni wilaya inayopakana katika mkoa wa Rukwa. Wilaya hii imekuwa maarufu kuliko hata mkoa wenyewe kulingana na historia, pamoja na matukio kadha wa kadha ya kishirikina yanayotokea katika wilaya hiyo.
Uchawi maarufu unaotumika Sumbawanga huwa ni uchawi wa radi, ambao waganga na wachawi huutumia kuwaadhibu wale wanao wakosea, hasahasa wezi. Pia historia ya kutisha ya Sumbawanga, ndiyo inaifanya sehemu hii kuogopeka na kutajwa kuwa na uchawi zaidi nchini Tanzania.
Kigoma, mkoa wa Kigoma unashika nafasi ya pili kwakuwa na uchawi zaidi nchini Tanzania. Hii nikwasababu ya matukio kadha wa kadha ya kishirikina yanayotokea mkoani humo kila kunapokucha. Kibondo ndiyo sehemu ambayo inatakiwa kuwa na uchawi zaidi mkoani humo.
Sinyanga/makao Makuu ya wachawi, mkoa huu pia umetajwa kuwa na uchawi zaidi nchini Tanzania. Matukio ya kishirikina katika mkoa huu, pia yamekuwa yakitokea kila kunapokucha. Miaka ya nyuma mauaji ya maarubino, na mauaji ya vikongwe wenye macho meusi yakuwa yakitokea mara kwa mara mkoani humo. Hii ndiyo sababu iliyoupa zaidi mkoa huu umaarufu mkubwa wa kuwa na uchawi zaidi.
Pia Katika mkoa huu wa Shinyanga, ndio mkoa ambao inasemekana kuwa makao Makuu ya wachawi Tanzania. Gamboshi jina la kijiji kinachopatikana mkoani humo, hususani Katika wilaya ya Simiyu, ndiko inasemekana kuwa na mambo mengi ya kichawi, mambo ambayo Kwa jicho la kawaida ni ngumu sana kuona, mpaka mtu mwenye nguvu za ziada.
CHANZO:Kaziforum
Comments
Post a Comment