MWANDISHI NYANDA HATIANI KUMLIPA DED UBUNGO BILIONI 2



Mwandishi wa habari kutoka Kampuni ya Sahara Media Group na mwendeshaji wa kipindi cha The Big Agenda Aloyce Nyanda ametiwa hatiani kwa kosa la kumdhalilisha mitandaoni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ubungo Aron Kagurumjuli.

Baada ya kutiwa hatiani Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Nyanda amemhukumu kumlipa fidia ya Sh.billioni mbili Mkurugenzi aliyedhalilisha katika moja ya machapisho yake mtandaoni.

Akisoma hukumu hiyo ya kesi ya madai ya udhalilishaji namba 6166/2024 leo Aprili 11, 2024, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Bonaventure Lema amesema baada ya kusikiliza mpande mbili Nyanda alikutwa na hatia ya kumdhalilisha Mkurugenzi huyo kupitia mitandao yake ya kijamii.

Amesema kosa hilo ni kinyume cha Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 kifungu cha 35.

Imeandikwa na Mwandishi Wetu,Mwanza

CHANZO CHA HABARI 
NIPASHE.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA