MAMA FEI TOTO AITIKISA YANGA, AMPELEKA MWANAE SIMBA
Nyota wa Klabu ya Azam, Feisal Salum 'Fei Toto' huenda akajiunga na klabu ya Simba mwishoni mwa msimu huu licha ya kutakiwa na klabu ya Yanga ambayo aliwahi kuitumikia kwa mafanikio makubwa kwa misimu kadhaa.
Taarifa hii imekuja mara baada ya Mchambuzi wa michezo kutoka E FM, Wilson Oruma, Aprili 8, kuweka wazi kuwa vita bado ni mbichi kwa vilabu vya Simba na Yanga kwenye harakati za kuhakikisha wanainasa saini ya Feisal Salum.
Katika sakata hilo, klabu ya Yanga imeonesha nia kubwa ya kutaka kunasa saini ya nyota huyo, lakini klabu ya Simba nayo imeonesha nia kubwa ya kumtaka nyota huyo kikosini ikiwa ni njia moja wapo ya kuboresha kikosi.
Licha ya Yanga kuonekana kuwa wapo tayari kutoa hadi nyumba, dili lake na Fei Toto limeonekana kuwa gumu baada ya mama mzazi wa mchezaji huyo kuingilia kati dili hilo. Ambapo imeripotiwa kuwa hataki arudi tena Yanga Kufuatia kile alichopitia klabuni hapo.
Ikumbukwe kuwa, kipindi Feisal Salum anaondoka Yanga kwenda Azam FC kulitokea na sintofahamu kubwa kiasi cha sakata lile kuamuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ndipo aliporuhusiwa na klabu hiyo kuondoka rasmi.
Jambo ambalo limeonekana kurahisisha dili la Fei Toto na klabu ya Simba. Pia, imeelezwa kuwa hata kwa upande wa Feisal anataka aende Simba kwa maana ndiyo klabu pekee kubwa ambayo bado hajaitumikia nchini.
Licha ya haya yote, kila kitu kitafahamika mwishoni mwa msimu kwenye dirisha kubwa la usajili, ambapo vilabu hivyo vitakuwa vina tangaza majina ya wachezaji wapya vikosini.
Je, unatamani kuona Fei Toto akivaa jezi ya timu gani msimu ujao? Karibu kwa maoni.
Chanzo:Mzee wa Jambia (IG)
Comments
Post a Comment