MWANAUME ACHA HIZI "K" TATU KUEPUKA UMASIKINI



Mwanaume ni mtu ambaye ameumbwa na mwenyezi mungu kwajili ya kuongoza dunia na vitu vyake vyote akiwema mwanamke ndani yake. Siku ya leo nakuletea "K" hizi tatu ambazo mwanaume akiziendekeza basi anaweza kuwa masikini wa kutupwa yeye na familia zake, lakini endapo akiziogopa basi anaweza kusahahu swala la umasikini kwenye maisha yake.

"K" ya kwanza ni kula sana. Mwanaume unapokua katika upo katika hali ya kujitafuta hutakiwi kuweka chakula kama kitu cha msingi sana. Hapa namaanisha mfano mwanaume umepata shilingi elfu 10 hakikisha unatumia kiasi kidogo kwenye chakula kuliko kinachobaki. Wataalamu wanasema kwamba endapo mwanaume utaweza kuondokana na dhana hii ya kula sana alafu ela yako kubwa ukawekeza kwenye mambo mengine, basi kuna asilimia kubwa sana ya wewe mwanaume kufanikiwa kwenye maisha yako.

Lakini ukitaka kuwa masikini wa kutupwa basi endekeza kula. Leo umepata elfu 20 unataka ukale chakula cha elfu 15 ubaki na robo ya ela hiyo. Lakini pia kumbuka hata mke wako nyumbani ukimwendekeza kula sana, siku chakula hakipo anaweza kukimbia familia kwani ataona humpendi yaani umebadirika.

"K" ya pili ni kuongea sana. Hakuna kitu kibaya kama mwanaume ukawa na tabia ya kuongea sana. Hii ni hatari sana kwenye maisha yako, kwani kuna wakati watu wanaweza kuogopa kukupa nafasi za kazi kwa kuogopa kuwa utawachoma. Zipo kazi zingine za wanaume zinahitaji siri sana, kwahiyo wakiona wewe huwezi kukaa na jambo yaani unaongea sana hapa lazima watakuweka pembeni tu.

Lakini pia wapo wanaume ambao wakifika nyumbani tu ni kuanza kuongea kwa kubwatuka mpaka mke anaogopa. Inasemekana kama kwamba mwanamke wako anaweza kushindwa kukuambia mawazo yake ambayo yuko nayo siku hiyo. Lakini pia kuongea sana kunaweza kufanya mtu ukashindwa kutekeleza mambo yako binafsi.

"K" ya mwisho, Mwanaume acha kulala sana. Wataalamu wanasema kwamba katakama hauna kazi ya kufanya, mwanaume hakikisha una masaa machache ya kulala. Tumia muda wako mwingi kutafuta kazi au kama una kazi basi fanya kazi kwa bidii sana. Ukiweza kuondokana na tabia ya kulala sana, basi kuna asilimia kubwa sana ya wewe kuwa tajiri maisha yako.

Mwanaume ni nguzo ya familia, hakuna budi kufata hizi "K" tatu, nilizokuketea hapa mpenzi msomaji wangu. Kama wewe ambaye unasoma hapa ni mwanaume basi yakupasa kushika mafundisho haya, kisha jaribu kuyafanyia kazi. Lakini pia kama wewe msomaji ni mwanamke na una kaka au mume basi unaweza mwambia mtu wako huyo asiache kusoma makala hii.

Lakini Je, wewe mpenzi msomaji wa habari hii, unalipi la kusema kuhusiana na "K" hizi tatu ? Lakini pia kama kuna "K" zingine unahisi zinaweza kuleta mabadiliko, tafadhali usisite kuziweka hapo chini kwenye maoni, ili watu wengine wazidi kupata elimu ya namna gani sisi wanaume tunaweza kuondokana na umasikini.

Chanzo: Wasafi Fm

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA