TUNDU LISSU AHAMISHIWA UKONGA GHAFLA



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa taarifa mpya kuhusu alipo Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu baada ya jana kueleza kuwa walienda kumtembelea Keko na hawakumpata

Chama hicho kimesema kuwa kinapenda kuuarifu umma kuwa mapema leo, tarehe 19 Aprili 2025, viongozi wakuu wa chama wamekutana na uongozi wa Jeshi la Magereza na kufahamishwa rasmi kuwa Mheshimiwa Tundu Lissu amehamishiwa katika Gereza la Ukonga.




Kufuatia taarifa hiyo, familia, wanachama wa CHADEMA na watanzania wote waliokuwa na wasiwasi kuhusu mahali alipo Mheshimiwa Lissu, wanataarifiwa kuwa sasa wanaweza kumtembelea kwa kufuata taratibu za kawaida za kumuona mahabusu katika Gereza hilo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chadema Brenda Rupia amesema kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara, Mheshimiwa John Heche, anatarajiwa kufika Gereza la Ukonga leo kwa ajili ya kumwona Mheshimiwa Tundu Lissu na kuzungumza naye kuhusu hali yake.

Jana Ijumaa Chadema walitoa taarifa kuwa viongozi wa Chama walifika Keko kumuona mwenyekiti wao lakini wakaelezwa kuwa
amehamishwa bila kuelezwa alipohamishiwa lakini sasa wanasema wameelezwa kuwa yupo Ukonga na wanaweza kwenda kumuona




Chadema wanaendelea na mikutano yake ya hadhara katika kanda ya Pwani ikiwemo Dar es salaam ambapo wameendelea kushinikiza kuachiwa kwa kiongozi huyo Mkuu wa Chama hicho na kuendelea na Majukumu yake ya siasa


Lissu alikamatwa Mkoani Ruvuma akiendelea na mikutano ya chama na kurejeshwa Dar es salaam ambapo alipandishwa kizimbani kwa makosa ya Uhaini pamoja na kusema uongo

Kesi yake inatarajiwa kitajwa April 24 jijini Dar es salaam ambapo itaanza kusikilizwa huku Chama hicho kikiwataka wanachama wao kujitokeza mahakamani hapo kumpa nguvu kiongozi huyo

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA