FUKUTO LA OBAMA NA TRUMP KUHUSU SERA YA UCHUMI

Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, ameonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu sera za Rais wa sasa, Donald Trump, tangu aanze muhula wake wa pili madarakani. Akizungumza katika Chuo cha Hamilton kilichopo jimboni New York siku ya Alhamisi, Obama alikosoa vikali sera za kiuchumi za Trump, juhudi za kupunguza matumizi ya serikali, msimamo dhidi ya wahamiaji, na namna anavyoshughulikia vyombo vya habari. Obama alilaani vikali hatua ya hivi karibuni ya Trump kuweka ushuru mkubwa kwa bidhaa kutoka kwa karibu washirika wote wa kibiashara wa Marekani, akisema “Sidhani kama kile tulichoshuhudia... kitakuwa na manufaa kwa Marekani.” Akiwa na umri wa miaka 63, mwanasiasa huyo wa chama cha Democratic alisema kuwa ingawa ushuru huo ni suala moja tu, ana wasiwasi mkubwa zaidi kuhusu hatua za serikali ya Trump kukandamiza uhuru wa wanafunzi wanaoshiriki maandamano ya kupigania haki za Wapalestina. Alieleza kuwa kitisho dhidi ya taasisi za elimu ya juu, shinikizo kwa kampuni za sheria, na kuzuia waandi...