MKUDE ACHEMSHA VIBAYA


                          Jonas Mkude


KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude, amekiri kuchemsha katika dili lake la kucheza soka la kulipwa katika Klabu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini, lakini akajipa moyo kuwa atautumia ujuzi alioupata katika majaribio yake kuibeba Simba kwenye Ligi Kuu Bara.
“Mambo hayajaenda sawa, najipanga upya,  lakini kile kichache nilichokipata kitakuwa fundisho kwangu kukifanyia kazi katika Ligi Kuu Bara, ingawa nimekosa kwa wakati huu, lakini ni tofauti na kutojaribu kabisa, hilo tu limenipa ujasiri wa mimi kujiamini kuwa ninaweza kufika mbali licha ya kipindi nilichokuwa nahitaji kukwama,” alisema.
Mbali na hilo alisema anajiunga na wenzake leo Jumanne hivyo akili yake anaielekeza kupokea mbinu mpya  kotoka kwa kocha,  Dylan Kerr.
 “Kila kocha anakuja na mbinu zake na wenzangu tayari wameanza kunolewa naye, lazima akili yangu itulie ili niendane na kile anachokitoa,” alisema.
Pia alisema ujio wa mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Hamis Kiiza, kikosini mwao unaongeza changamoto.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA