BIASHARA YA NGONO YASHAMIRI DODOMA, MAKAHABA WAJAZANA KILA KONA



BIASHARA ya ngono imeshamiri mkoani Dodoma wakati huu ambao vikao vya kumpata mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) vimekwisha kuanza.
 
Uchunguzi uliofanywa  katika baadhi ya kumbi kama  Club Maisha, Club Laazizi na Matei Lounge, Chako ni Chako, umebaini kuwapo idadi kubwa ya kina dada wakiwa wamevaa nusu uchi.
 
Katika maeneo ya katikati ya mji wa Dodoma zilikuwapo hekaheka za wasichana wanaojiuza ambao walionekana wakitafuta wateja bila ya wasiwasi wowote na wengine walisikika wakisema  wako kibiashara na siyo kuuza sura.
 
Eneo maarufu la Chako ni Chako kuanzia jioni mpaka usiku kucha  akina dada hao wamekuwa wakijazana hadi kwenye taa za kuongozea magari huku wakitafuta wateja wenye magari.
 
Baadhi yao ambao hawakutaka kutaja majina yao halisi mmoja wao alisema, ‘’Kaka sema una shilingi ngapi habari ya majina unataka kutupeleka wapi…?
 
‘’……wewe unaona shimo limetema hapa kila nikigeuka mwanaume na wanatoa ‘mpunga’ nadhani huyu rais ajaye atakuwa na neema.’’
 
Dada mwingine ambaye aliyekuwa   Dodoma Carnival karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi, alisema ametoka Arusha akiwa na marafiki zake kwa lengo la kuwafuata wateja wa msimu walioko Dodoma.
 
Alisema hadi sasa ana   siku tatu akiwa  Dodoma na tayari amekusanya zaidi ya Sh 700,000 huku akiwatumia madalali  ambao huwaunganisha kwa wateja ‘wazito’ (wenye fedha) kwa ujira maalum.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA