Skip to main content

ZITTO AHAMIA RASMI ACT NA KUKABIDHIWA KADI



Mh. Zitto Kabwe akilipa kwa ajili ya usajili wa kadi ya uanachama wa ACT...
Hayawi hayawi… Sasa yamekuwa! Licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe sasa yamekuwa kweli kwa Mbunge huyo baada ya leo Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.

Hii inafuatia siku moja baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi kuendeleza mapambano ndani ya
 chama hicho.


Mh. Zitto Kabwe akisaini kadi ya uanachama wa ACT.Hata hivyo, kwa mujibu wa viongozi 

waandamizi wa ACT-Tanzania wamedokeza kuwa, Zitto ataongea na vyombo vya habari
Jumapili ya Machi 22. 

NB: ACT-Tanzania: kirefu chake ni : Chama cha Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania). Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.


Mh. Zitto Kabwe akikabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa ACT.

Mwanachama rasmi wa ACT, Mh. Zitto Kabwe akipokea kadi hiyo.
“He..he he mnipokeee sasa kwa mikono miwili….:, Mh. Zitto Kabwe akionyesha kadi hiyo 


Mh. Zitto Kabwe akibadilishana mawazo na viongozi wa Chama cha ACT mara baada ya
kupokea kadi hiyo.


Mh. Zitto Kabwe akiwa amefuatana na Prof. Kitila Mkumbo ambaye pia ni mwanachama wa ACT.

Mh.Zitto Kabwe akivalishwa skafu ya ACT mara baada ya kupokea rasmi kadi ya chama 
hicho mapema leo.

Na hii ndio kadi rasmi ya Mheshimiwa Zitto Kabwe aliyokabidhiwa leo.

Chanzo: MO Dewji Blog

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA