KESI ALIYOIFUNGUA ZITTO DHIDI YA CHADEMA YAFUTWA, ZITTO ATAKIWA KULIPA GHARAMA ZA KESI




MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, leo imetupilia mbali shauri lililofunguliwa na Zitto Zubeir Kabwe mwaka jana, akipinga kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kumjadili, akikitaka chombo hicho cha sheria, kukielekeza chama chake, kusubiri kwanza rufaa yake aliyokuwa amekata katika Baraza Kuu.
Mahakama iliyoketi chini ya Jaji Mziray, ilikubaliana na hoja za mawakili wa Chadema, waliosema kuwa ufunguaji wa kesi hiyo ulikiuka baadhi ya vifungu vya sheria na hivyo kumtaka mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kulipa gharama zote za kesi hiyo.
Wakati Zitto akifungua kesi hiyo Januari mwaka juzi, tayari Chadema ilikuwa imewafukuza uanachama Dr. Kitilya Mkumbo na Samson Mwigamba ambao pamoja na Zitto, walituhumiwa kupanga njama za kufanya mapinduzi ya uongozi ndani ya chama hicho. Zitto alikuwa akitetewa na wakili Albert Msando wakati Chadema iliwakilishwa na Tundu Lissu, Peter Kibatala na John Mallya.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA