MCHUNGAJI NIGERIA AWAPA MIMBA WANAWAKE 20 AKIDAI NI AGIZO LA ROHO MTAKATIFU

mimba

Mchungaji mmoja nchini Nigeria, amekamatwa kwa udhalilishaji baada ya kuwapa ujauzito waumini wake zaidi ya 20 kati yao wakiwa katika ndoa na wasichana wadogo kwa madai ni maagizo aliyopewa na Roho Mtakatifu.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Ebere Amaraizu, amekiri kukamatwa kwa mchungaji Timoth Ngwu, wa kanisa la Vineyard Ministry of the Holy Trinity, ambaye alikuwa akiwa akiwatumia vibaya kimapenzi wanawake na wasichana wadogo wa kanisa lake.
Mchungaji huyo amesema kuwa alikuwa akifuata matakwa aliyopewa na Roho Mtakatifu ya kumpa ujauzito mtu yeyote ambaye amechaguliwa na kuoneshwa na Roho huyo haijalishi mwanamke huyo ameolewa au hajaolewa.
Inasemekana kuwa mwanamke akipata ujauzito na kujifungua hubaki na mtoto wake katika eneo hilo la mchungaji maisha yake yote baada ya kuwa wamekubaliana na mume wake.
Kaka wa mchungaji huyo amesema kuwa, alikuwa akimuonya sana Ngwu, kuhusu tabia yake lakini alikuwa hataki kumsikiliza na kuongeza kuwa Calista Omeje na Assumpta Odo, waliweza kuwaacha waume zao na kukubali kuishi na mchungaji huyo kwa madai kuwa ameoneshwa na Roho Mtakatifu.
Aidha, Odo, alitoa ushahidi kuwa mchungaji huyo aliweza kuzaa naye mtoto mmoja ambaye bahati mbaya alipoteza maisha na kukiri kuwa mchungaji huyo aliweza pia kumzalisha binti yake.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA