Posts

Showing posts from March, 2015

GWAJIMA AJISALIMISHA POLISI

Image
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima amejisalimisha kituo cha polisi kati kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo. Mchungaji Gwajima anatuhumiwa kumkashifu na kumtukana hadharani Kardinali Pengo.    Matusi hayo   ni  yale yaliyoonekana kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii  ambapo kuna sauti iliyorekodiwa na picha za video zikimuonyesha Mchungaji Gwajima akimkashifu na kumtukana kwa maneno makali Kardinali Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine. Hata  hivyo, mapema  leo  Asubuhi, kipande cha  sauti   ya  Gwajima kilisambaa   katika  mitandao  mbalimbali  ya  kijamii  kikidai kuwa Gwajima angejisalimisha Polisi Jumatatu kwa kuwa kwa sasa yupo Arusha na kuwataka waumini wake kufika polisi Jumatatu bila kufanya vurugu. Haijafahamika  mar...

MGOGORO NDANI YA CHAMA CHA ACT WANUKIA, MWENYEKITI ALIYETIMULIWA AMLAUMU ZITTO

Image
SAKATA la uongozi ndani ya Chama cha Mabadiliko na Uwazi (ACT-Tanzania), limeendelea kuchukua sura mpya baada ya uongozi uliodaiwa kuvuliwa madaraka, kudai Bw. Zitto Kabwe ndiye aliyesababisha mgogoro katika chama chao. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Kadawi Limbu alisema chanzo cha mgogoro unaoendelea katika chama hicho ni Bw. Kabwe ambaye awali hakuwa mwanachama halali; lakini alipanga mikakati yote nje ya chama. Alisema mikakati mingi ya chama hicho ilipangwa nyumbani kwa Bw. Kabwe na watu watatu akiwemo Profesa Kitila Mkumbo na Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Samson Mwigamba bila yeye kama kiongozi (Limbu) kujulishwa. "Nipo tayari kufa hadi haki ipatikane, mimi ndiye kiongozi wa ACT-Tanzania, mara ya mwisho kuwasiliana na Bw. Kabwe ni Desemba 10, 2014, barua kutoka kwa Msajili Siasa ya Februari 27, 2015 kwenda kwa Katibu Mkuu wa chama, alisema yeye ametoa ushauri si maelekezo. "Ushauri wake tu...

LOWASA : TUHUMA ZA KUWALIPA WATU WANISHAWISHI KUGOMBEA URAIS NI UPUUZI NA UONGO

Image
Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, amesema watu wanaosema anawalipa watu wanaomshawishi awanie nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, ni upuuzi na uongo na kwamba hawezi kuwajibu kwani kufanya hivyo ni kuwapa sifa wasizostahili. Lowassa aliyasema hayo nyumbani kwake jana mjini Dodoma, kufuatia baadhi ya vyombo vya habari, kumnukuu Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, ambaye ametangaza nia ya kuwania urais, akisema baadhi ya watu wanatumia vibaya umaskini wa Watanzania kwa kuwakusanya na kuwapa fedha ili waseme wanawashawishi wawanie urais. Akizungumza mbele ya wachungaji 110 wa makanisa ya Kipentekoste kutoka sehemu mbalimbali nchini jana, Lowassa alisema hana uwezo wala sababu ya kuwagharimia watu wanaofika nyumbani kwake kumshawishi na kwamba wengi wanafanya hivyo kwa mapenzi yao na Mungu wao. “Najiunga na mwenzangu (Mwenyekiti wa CCM Shinyanga, Khamis Mgeja) kusema leo (jana) kuna mtu kwenye magazeti amesema maneno ya hovyo ...

MVUA YAUWA WATANO DAR

Image
HALI ni tete katika jiji la Dar es Salaam, kutokana na mvua ya masika iliyonyeshwa kwa siku tatu na kusababisha vifo vya watu watano, huku nyumba nyingi zikiwa zimezingirwa na maji.   Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Buguruni kwa Mnyamani na eneo la Jangwani katika Manispaa ya Ilala, ambako nyumba nyingi na barabara zimeathirika.   Sehemu nyingine za jiji zimezingirwa na maji kutokana na kuziba kwa mitaro na mifereji, ikiwa ni athari ya utupaji taka ovyo na pia miundombinu duni.   Hata hivyo, kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), mvua kubwa zaidi zinatarajia kuendelea kunyesha mpaka Jumatano.   Kutokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha, Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (pichani) jana aliongoza kikosi cha uokoaji katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani, ambako nyumba 250 zilizingirwa na maji, jambo ambalo vikosi vya uokoaji vililazimika kufanya kazi ya kuwanasua watu waliokuwa wamekwama katika nyumba zao.   ...

ZITTO AHAMIA RASMI ACT NA KUKABIDHIWA KADI

Image
Mh. Zitto Kabwe akilipa kwa ajili ya usajili wa kadi ya uanachama wa ACT. .. Hayawi hayawi… Sasa yamekuwa! Licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe sasa yamekuwa kweli kwa Mbunge huyo baada ya leo Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194. Hii inafuatia siku moja baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi kuendeleza mapambano ndani ya  chama hicho. Mh. Zitto Kabwe akisaini kadi ya uanachama wa ACT.Hata hivyo, kwa mujibu wa viongozi  waandamizi wa ACT-Tanzania wamedokeza kuwa, Zitto ataongea na vyombo vya habari Jumapili ya Machi 22.  NB: ACT-Tanzania: kirefu chake ni : Chama cha Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania). Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania. Mh. Z...

ZITTO KABWE KULIPWA MAFAO YAKE

Image
Ikiwa ni siku moja tangu Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutangaza kung’atuka katika nafasi yake ya ubunge, Bunge limeeleza kuwa mbunge huyo atapata mafao yake yote kama wabunge wengine.   Zitto ambaye alitangaza juzi bungeni kuwa anaondoka baada ya kuvuliwa unanachama wa Chadema aliahidi kuwa ‘Mungu akipenda’ atakuwa tena ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria Novemba mwaka huu baada ya uchaguzi mkuu.   Kuondoka kwa mbunge huyo pia kunaifanya nafasi ya uenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali(PAC) kuwa wazi kwa kuwa ndiye aliyekuwa akiishikilia hadi alipotangaza rasmi juzi kuachia ubunge.   Akizungumzia uamuzi wa Zitto na juu ya mafao yake baada ya kuamua kuondoka mwenyewe, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alisema kuwa mbunge huyo atalipwa mafao yake yote.   “Unajua Chadema wametangaza kumvua uanachama Zitto lakini hawajampa barua, sasa yeye ameona kuwa kuliko kuendelea na ubunge wake ni vyema akakaa kando. Kutokana na suala hilo atal...

BARUA YA MH. ZITTO YA KUNG'ATUKA UBUNGE

Image

HOTUBA YA MH ZITTO KABWE ILIYOKUWA ISOMWE BUNGENI ALHAMISI MACHI 19 HII HAPA

Image
MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBEIR KABWE, MB KUHUSU UANACHAMA WAKE KATIKA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) NA HATMA YAKE KAMA MBUNGE KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. DODOMA, ALHAMISI 19 MACHI 2015. 1. Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana kwa fursa uliyonipa kutoa maelezo yangu binafsi katika Bunge lako Tukufu leo. Ninatoa maelezo haya kwa mujibu wa Kifungu cha 50 (1) cha Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013 kinachosema kwamba, “Mbunge yeyote anaweza, kwa idhini ya Spika, kutoa maelezo binafsi Bungeni yanayolenga kufafanua kuhusu jambo lolote linalomhusu na lililoifikia jamii” 2. Mheshimiwa Spika, Nilijiunga na Bunge lako Tukufu kwa mara ya kwanza Mwaka 2015 nikiwa na lengo kuu la kupaza sauti ya vijana kwenye masuala yanayohusu nchi yetu na kutetea maslahi ya Watanzania hususani Wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Mkoa wa Kigoma, na Watanzania kwa ujumla. Nilichaguliwa na wananchi wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia n...

MTOTO WA MWAKA MMOJA ALIVYONUSURIKA KWENYE AJALI YA BASI LA MAJINJA- MAFINGA

Image
Mtoto aliyenusurika kwenye ajali. BADO Mji wa Mafinga wilayani Mufindi mkoani hapa haujakaa sawa kufuatia vifo vya watu 50 waliopoteza maisha kwa ajali ya kontena kudondokea Basi la Majinja lenye namba za usajili T 438 CED iliyotokea Machi 11, 2015, Uwazi limechimbaAjali hiyo ilitokea maeneo ya Changarawe mjini Mafinga ambapo kontena hilo lilikuwa kwenye lori la mizigo la Scania lenye namba za usajili T 689 APJ mali ya Kampuni ya Cipex lililokuwa likitokea Dar kwenda Mbeya huku basi hilo likitokea Mbeya kuelekea Dar. KILICHOTOKEA BAADA YA AJALI Kilichotokea baada ya ajali hiyo ni kuonekana kwa Mkono wa Mungu ambapo mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja mpaka miwili kunusurika katika ajali hiyo huku watu 50 wakipoteza maisha. “Mimi naweza kusema ni Mkono wa Mungu kwa sababu, yule mtoto alikutwa hajaumia popote lakini wazazi wake wakiwa wamepoteza maisha. Huoni kama ni uwezo wa Mungu mwenyewe?” alisema askari polisi mmoja aliyekuwa miongoni mwa walio...