RAIS MAGUFULI AMTEUA CHIKAWE KUWA BALOZI WA JAPAN



Rais John Magufuli amemteua Mathias Chikawe kuwa balozi wa Tanzania  nchini Japan.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Mathias Chikawe kuwa balozi wa Tanzania  nchini Japan.

Taarifa iliyotolewa leo 18 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Chikawe umeanza Aprili 13, 2016.

Kabla ya kupangiwa kituo hicho cha kazi, Chikawe aliteuliwa kuwa Balozi mnamo Februari 15, 2016.

Chikawe aliwahi kuwa mbunge wa  Nachingwea kati ya Mwaka 2005 na 2015, na kwa vipindi tofauti katika serikali ya awamu ya nne alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA