MABADILIKO YA MATUMIZI YA DARAJA LA KIGAMBONI LEO


Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya ufunguzi wa Daraja la Kigamboni leo, Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016.Kutokana na ufunguzi huo, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataarifu watumiaji barabara na Wananchi wote wanaotumia daraja hilo kuwa huduma ya magari kutumia daraja hilo itafungwa kwa muda kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana ili kuwezesha kufanyika kwa sherehe hiyo ya ufunguzi wa daraja. Aidha, huduma katika Daraja la Kigamboni itarejea kama kawaida kuanzia saa 8:00.Daraja la Kigamboni lililoanza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 lina urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5.Imetolewa na;Eng. Joseph M. NyamhangaKatibu Mkuu (Ujenzi)Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano18 Aprili, 2016.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA