BUNGENI: TANI MILIONI MBILI ZA MUHOGO ZAUZWA KWA DOLA NCHINI CHINA





Serikali imepata soko nchini China, kupeleka tani milioni 2 za mihogo zenye thamani ya Dola 300 milioni za Marekani.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana  na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masalla (CCM). 

Masalla alitaka kufahamu jitihada za Serikali katika kuwatafutia wakulima nchini masoko ya mazao yao.

Akijibu swali hilo, Mwijage alisema mbunge huyo amewahisha masuala ya bajeti ijayo na kwamba, Serikali tayari imepata soko la mihogo nchini China.

Awali, Mbunge wa Viti Maalumu, Hamida Mohamed Abdallah (CCM) alitaka kujua Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda ya Mwaka 1996-2020, jinsi inayolenga kuvifanya viwanda vya usindikaji mazao kuongeza thamani na kukuza uchumi.  

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA