Posts
Showing posts from April, 2016
THE SOW BAND - UNYENYEKEVU
- Get link
- X
- Other Apps
Bwana Yesu asifiwe ndugu zetu Watanzania, sisi ni watoto wenu/wadogo zenu/ kaka zenu kutoka Tanga, tumeokoka tunampenda Yesu, na ndio maana tumeamua kumtumikia yeye katika kumsifu na kumuabudu, Tunaimba muziki wa Bendi, na yetu inafahamika kwa jina la THE SOW BAND ambapo ni kifupi cha SOUL OF WORSHIP. Hivyo basi, tunapoanza kutoa sigle yetu ya kwanza ambayo ni hii inayokwenda kwa jina la UNYENYEKEVU ambayo ipo katika mtindo wa Bolingo (sebene) tunaomba mtupokee na tunaomba mchango wako kwa kwa kutembelea Youtube na kusikiliza audio yetu, kwako wewe kutembelea youtube ni jambo dogo ila kwetu utakuwa umetufanyia kitu kikubwa sana tafadhali usiache kutembelea youtube tunahitaji sana mchango wako bila hakuna THE SOW BAND. Asante sana na Mungu akubariki.
MKATABA TATA WA LUGUMI WATUA BUNGENI
- Get link
- X
- Other Apps
Hatima ya mkataba tata wa kampuni ya Lugumi Enterprises ipo mikononi mwa Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya jana, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwasilisha muhtasari wa ilichokibaini baada ya kupitia maelezo ya utekelezaji wake. Moja kati ya mambo yaliyomo katika muhtasari huo ni kulitaka Bunge kutoa ruhusa kwa kamati ndogo iliyoundwa na PAC juzi kuchunguza kwa kina mkataba huo wa kufunga mtambo wa utambuzi wa vidole (AFIS), ikiwa ni pamoja na kutembelea vituo vinavyodaiwa kufungwa mashine hizo. Kamati ya PAC ilinusa ufisadi kwenye mkataba huo wa AFIS ulioitaka Lugumi kufunga mitambo kwenye vituo vya polisi 108 kwa gharama ya Sh37 bilioni lakini ilibainika kwamba kampuni hiyo ililipwa kiasi cha Sh34 bilioni zaidi ya asilimia 90 ya fedha zote ilhali imefunga mashine 14 tu mkoani Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hilaly alisema jana muda mfupi baada ya kukutana na ...
HATARI SANA :MCHEZA FILAMU ZA NGONO ALIYEFARIKI AITWA SHUJAA
- Get link
- X
- Other Apps
Aliyekuwa mchezaji mieleka na nyota wa filamu za ngono Chyna amefariki akiwa na umri wa miaka 45. Meneja wake amethibitisha habari hiyo kupitia mtandao wake wa Twitter. ''Ni masikitiko makubwa kutangaza kwamba tumempoteza shujaa'',ulisema ujumbe huo,akiongezea kuwa:Ataishi kukumbukwa na mashabiki wake wengi na sisi sote tuliompenda. Chyna alipatikana amefariki nyumbani kwake katika ufukwe wa bahari wa Redondo,mjini California,baada ya kurudi nyumbani kutoka Japan. Chyna alipochumbiwa na mchezaji mwenza wa miereka Mapema wiki hii alichapisha kanda ya video yenye urefu wa dakika 13 ambapo anazungumza kuhusu kuanzisha biashara mpya ya chakula. Alionekana akikosea baadhi ya maneno aliyokuwa akiyatamka na anaonekana amechanganyikiwa. Alijitahidi kukabiliana na dawa za kulevya wakati wote wa kazi yake na alionekana katika kituo cha kuwarekebisha tabia watu maarufu mwaka 2008.
MSANII BONGO MOVIES AFARIKI AKIJIFUNGUA
- Get link
- X
- Other Apps
DAR ES SALAAM : Ni simanzi! Nyota ya msanii Leila Gabriel ‘Lissa’ ambayo ndiyo kwanza ilikuwa imeanza kuchomoza kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, ilizimika ghafla mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya msanii huyo kupoteza maisha muda mfupi baada ya kujifungua kwenye Hospitali ya St. Benard, Kariakoo jijini Dar es Salaam. Filamu alizowahi kucheza? Aishiwa nguvu wakati wa kujifungua. Aabainika kutokuwa na damu ya kutosha. Madaktari washindwa kumfanyia upasuaji Bahati nzuri ajifungua salama. Apatwa balaa lingine baada ya kujifungua, afariki dunia. Mama wa Marehemu afunguka mazito kuhusu kifo cha mwanaye. Simulizi ya kifo chake inasikitisha sana! “Inauma sana, mwanangu amefariki kwa maumivu maana shida ilikuwa ni ambulance, kama ingepatikana kwa wakati naamini angepona lakini ndiyo hivyo tena, kazi ya Mungu haina makosa,” alisema mama h...
NAIBU MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUPATIKANA LEO
- Get link
- X
- Other Apps
Meya wa jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, anatarajiwa kupatikana leo katika kikao cha kwanza cha Baraza la Jiji kitakachofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee. Uchaguzi wa naibu meya unafanyika baada ya kukamilika kwa mchakato wa kumpata meya wa jiji hilo uliohitimishwa Machi 22, mwaka huu kufuatia kutawaliwa na ‘figisufigisu’ kati ya CCM na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) zilizosababisha uaharishwe mara tatu. Katika kinya’nga’nyiro hicho, Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema), Isaya Mwita aliibuka kidedea kwa kupata kura 84 dhidi ya Diwani wa Kata ya Mburahati (CCM), Yusuph Yenga aliyepata kura 67. Meya wa jiji hilo, Isaya Mwita jana alisema kuwa, maandalizi ya kikao hicho kitakachokuwa na ajenda ya uchaguzi wa kumpata naibu meya yamekamilika. Wagombea nafasi hiyo ni Kafana Mussa wa (CUF) na Mariam Lulida wa CCM. Tofauti na uchaguzi wa meya, uchaguzi wa leo hautarajiwi kuwa na mvutano mkubwa b...
BUNGENI: TANI MILIONI MBILI ZA MUHOGO ZAUZWA KWA DOLA NCHINI CHINA
- Get link
- X
- Other Apps
Serikali imepata soko nchini China, kupeleka tani milioni 2 za mihogo zenye thamani ya Dola 300 milioni za Marekani. Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masalla (CCM). Masalla alitaka kufahamu jitihada za Serikali katika kuwatafutia wakulima nchini masoko ya mazao yao. Akijibu swali hilo, Mwijage alisema mbunge huyo amewahisha masuala ya bajeti ijayo na kwamba, Serikali tayari imepata soko la mihogo nchini China. Awali, Mbunge wa Viti Maalumu, Hamida Mohamed Abdallah (CCM) alitaka kujua Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda ya Mwaka 1996-2020, jinsi inayolenga kuvifanya viwanda vya usindikaji mazao kuongeza thamani na kukuza uchumi.
BUNGENI: MPANGO WA PILI WA MAENDELEO WA TAIFA WWASILISHWA BUNGENI ...TRILIONI 107 ZAHITAJIKA KUTEKELEZA MPANGO HUO
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango Shilingi trilioni 107 zinahitajika kugharamia utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2016/21, ambao utategemea sana makusanyo ya kodi na ukijikita katika kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda. Akiwasilisha bungeni jana Mpango huo wa Pili wa Maendeleo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango alisema katika fedha hizo, Sh trilioni 59 zitatolewa na serikali, huku kiasi kilichobaki cha Sh trilioni 48 zitachangiwa na sekta binafsi pamoja na mikopo na misaada kutoka nje. Akitoa mchanganuo wa ugharamiaji mpango huo, Dk Mpango alisema kila mwaka serikali itatoa Sh trilioni 11.8 na kwamba katika kipindi cha miaka mitano ya mpango huo, serikali itakuwa imetoa jumla ya Sh trilioni 59. Alisema eneo la pili la gharama za mpango huo, litabebwa na sekta binafsi, mkopo na misaada kutoka nje na kuwa serikali inaweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi kuwekeza kati...
RAIS MAGUFULI AMTEUA CHIKAWE KUWA BALOZI WA JAPAN
- Get link
- X
- Other Apps
Rais John Magufuli amemteua Mathias Chikawe kuwa balozi wa Tanzania nchini Japan. Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Mathias Chikawe kuwa balozi wa Tanzania nchini Japan. Taarifa iliyotolewa leo 18 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Chikawe umeanza Aprili 13, 2016. Kabla ya kupangiwa kituo hicho cha kazi, Chikawe aliteuliwa kuwa Balozi mnamo Februari 15, 2016. Chikawe aliwahi kuwa mbunge wa Nachingwea kati ya Mwaka 2005 na 2015, na kwa vipindi tofauti katika serikali ya awamu ya nne alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
TANZIA: ALIYEKUWA MKURUGENZI WA BOT AMATUS LIYUMBA AFARIKI DUNIA
- Get link
- X
- Other Apps
MABADILIKO YA MATUMIZI YA DARAJA LA KIGAMBONI LEO
- Get link
- X
- Other Apps
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya ufunguzi wa Daraja la Kigamboni leo, Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016. Kutokana na ufunguzi huo, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataarifu watumiaji barabara na Wananchi wote wanaotumia daraja hilo kuwa huduma ya magari kutumia daraja hilo itafungwa kwa muda kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana ili kuwezesha kufanyika kwa sherehe hiyo ya ufunguzi wa daraja. Aidha, huduma katika Daraja la Kigamboni itarejea kama kawaida kuanzia saa 8:00. Daraja la Kigamboni lililoanza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 lina urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5. Imetolewa na; Eng. Joseph M. Nyamhanga Katibu Mkuu (Ujenzi) Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano 18 Aprili, 2016.
RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MAKUTANO YA BARABARA YA NYERERE NA MANDELA JIJINI DAR LEO
- Get link
- X
- Other Apps
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale akitoa maelezo kwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi ujwenzi wa Barabara ya Juu (FlyOver) kwenye makutano ya Barabara ya Mandela na Nyerere, eneo la Tazara, Jijini Dar es salaam leo. **** Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli ameweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza rasmi ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Nyerere na Mandela eneo la Tazara jijini Dar es Salaam leo. Akizungumza katika uzinduzi huo, Rais Magufuli amesema ujenzi huo wa barabara ya juu utaanza mara moja kwa ushirikiano na serikali ya Japan na utagharimu Shilingi 100 bilioni. Amesema, serikali ya Japan imefadhili mradi huo kwa Sh 93.44 bilioni wakati serikali ya Tanzania imechangia Sh 8.36 bilioni. Rais amewataka wananchi watakaopata ajira kwenye ujenzi wa mradi huo wawe...